Waziri mkuu wa Libya
ameachiliwa saa chache baada ya kutekwa nyara na watu wanaominika kuwa
wapiganaji wa kiisilamu. Hii ni kwa mujibu wa serikali ya Libya.
Ali Zeidan alitekwa nyara na kundi la
waasi waliokuwa na uhusiano na serikali kwa jina Revolutionaries Operations
Room.
Walisema walimteka nyara kwa maagizo
ya mwendesha mkuu wa mashtka ingawa wizara ya sheria imekanusha madai hayo.
Kundi hilo lilikuwa miongoni mwa makundi ya
wapiganaji walioghadhabishwa na hatua ya makomandao wa Marekani kumkamata Anas
Al-Liby mshukiwa wa kundi la kigaidi la al-Qaeda.
Wengi walitaja hatua ya Marekani kama
ya kuingilia uhuru wa taifa hilo
na kata kutaka maelezo kutoka kwa balozi wa Marekani nchini humo.
Mwandishi wa BBC mjini humo anasema
Zeidan alitekwa nyara akiwa ndani ya hoteli ya kifahari anamoishi.
Serikali imekuwa ikikabiliwa na
shinikizo kali baada ya makomando wa Marekani kumkamata mmoja wa viongozi wa
al-Qaeda Anas al-Liby nchini Libya.
Bwana Liby alikamatwa Jumamosi mjini Tripoli kwa madai ya kuhusika na mashambulizi ya kigaidi
yaliyofanywa dhidi ya balozi za Marekani nchini Tanzania
na Kenya
mwaka 2008.
Mnamo siku ya Jumatatu Libya ilimhoji
balozi wa Marekani kuhusu kukamatwa Al Liby.
Kwa upande wake Zeidan alitoa wito
kwa Marekani na nchi za Magharibi kuisaidia serikali ya Libya kukomesha
vitendo vya wapiganaji wenye itikadi kali nchini humo.
Kwenye mahojiano na BBC, alisema kuwa
Libya inatumiwa kama kambi ya kuweka silaha.
Waziri mkuu aliambia BBC kuwa nchi
yake inatumia kama kivukio cha kusafirishia
silaha kwenda katika maeneo mengine ya kanda hiyo.
No comments:
Post a Comment