Wananchi wa jimbo lenye mzozo la Abyei wamepiga kura ya kujiunga na
Sudan Kusini katika kura isiyo rasmi ya maoni iliyopigwa na kabila moja kati
makabila makuu mawili ya nchi hiyo.
Msemaji
wa Kamati inayosimamia kura hiyo ya maoni amesema asilimia 98.9 ya waliopiga
kura kutoka kabila la Ngok Dinka wamepiga kura ya kukubali kuijiunga na Sudan
Kusini.
Wanachama
wa Arab Misseriya ambao wana mshikamano na Sudan wamekataa kupiga kura hiyo na
kusema hawatatambua matokeo hayo.
Umoja
wa Afrika umeelezea kura hiyo maoni kuwa tishio la amani kati Sudan na Sudan Kusini.
No comments:
Post a Comment