Wednesday, October 30, 2013

Marekani yaongeza juhudi kumsaka Kony



Ripoti mpya inasema Marekani imeongeza  juhudi zake  kusaidia kumkamata mtoro  kiongozi wa kundi la waasi wa wa Uganda Joseph Kony Kwa mujibu wa gazeti la  Washington Post jeshi la Marekani limeomba White House kuweka kwa muda mfupi ndege aina ya Osprey nchini Uganda.

Inasema ndege aina hiyo inaweza kutua kama helikopta na kupaa kama ndege kubwa na itasaidia wanajeshi wa Marekani kwa ushirikiano na wenzao wa Afrika kumsaka Kony katika eneo kubwa analodhaniwa kuwa amejificha na kubomoa kambi alizoweka .

Washington Post linasema endapo ombi hilo litakubaliwa, idadi ya wanajeshi wa Marekani nchini Uganda itaongezeka maradufu na kufikia 100.
Uganda inaongoza juhudi za ukanda huo kumkamata Kony ambaye kundi lake la waasi Lords’ Resistance Army, limehangaisha vijiji vya nchi za Afrika ya kati kwa miaka.

 Aidha gazeti hilo linasema majeshi ya Marekani yameongeza mafunzo kwa wanajeshi wa Sudan Kusini  na  Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, ambayo yanahusika na msako dhidi ya Kony anayedhaniwa kuwa amejificha huko Congo.
Chanzo: VOASwahili

No comments: