KIUNGO Yaya Toure amekumbana na
kejeli za kibaguzi akifananishwa na nyani usiku huu Manchester City ikiibuka na
ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya CSKA Moscow katika Jiji Kuu la Urusi.
Kelele za kibaguzi zilisikika kutoka
mashabiki wa wenyeji katika mchezo ambao City ilinufaika na mabao mawili ya
Sergio Aguero ikitoka nyuma na kushinda mechi hiyo ya Li ya Mabingwa Ulaya.
Na City imethibitisha itapeleka
malalamiko rasmi UEFA juu ya 'unyama' aliofanyiwa Toure.
"Hakika inaumiza mtu
unapozungumza na watu wanaendelea kufanya hivyo,"alilalamika Toure.
"Huwezi kuamini na inaniumiza sana upande wangu,".
"Nafikiri UEFA wanahitaji kufanya
kitu cha nguvu. Itakuwa vizuri ikiwa watazuia hiyo.
"Baadhi ya nyimbo zilizokuwa
zinaimbwa zilikuwa za kipumabvu kabisa, nafikiri UEFA wanatakiwa kufanya kazi.
Kila wakati tunasema kitu fulani na inaendelea, kitu fulani lazima kifanyika
kuzuia hii,".
Alipoulizwa ni hatua gani ichukuliwe
na bodi hiyo ya soka Ulaya, Toure alitaka adhabu zitolewe badala ya faini ndogo
ndogo ambazo zimekuwa zikitolewa siku za nyuma.
"Wanahitaji kufanya
zaidi,"alisema. "Nafikiri UEFA wanatakiwa kuwa na nguvu, na kuzishika
klabu zote na mashabiki wote wanaofanya hivyo (wahusika). Labda kufungia
viwanja,".
"Kwangu kama mchezaji wa Afrikan
wakati wote imezungumzwa kusikia kwamba mambo kama hayo tunahitaji kufanya kitu
juu ya hilo,".
Chanzo: binzubeiry
No comments:
Post a Comment