Wanajeshi wa DRC wamefanikiwa
kuwatimua waasi wa M23 kutoka katika ngome yao kuu katika eneo la Bunagana.
Wanajeshi hao wamekomboa mji wa
Bunagana kufuatia makabiliano makali adhuhuri ya leo ambapo baadhi ya waasi
walilazimika kuimbilia msituni huku baadhi wakidai waliingia Uganda baada ya
kuvalia mavazi ya kiraia.
Msemaji wa serikali alisema kuwa mji
wa Bunagana ulio katika mpaka wa Uganda na DRC, sasa uko chini ya wanajeshi wa
serikali.
Wenyeji wa mji huo walithibitishia
BBC kuwa mji huo ulikombolewa na kuwa waasi wamekuwa wakitoroka mapambano
makali dhidi yao.
Hatua hii ya wanajeshi ni sehemu ya
ushindi mkubwa ambao wanajeshi wamekuwa wakiupata dhidi ya waasi hao wa M23
walianza harakati zao dhidi ya serikali ya Congo mwaka jana wakidaiwa kusaidiwa
na serikali ya Rwanda.
Mnamo siku ya Jumatatu mjumbe maalum
wa M23 hawana tena nguvu za kijeshi kwani sio tesho tena.,
Umoja wa Mataifa umesema kuwa
wakimbizi elfu tano wamelazimika kutoroka Bunagana na kuingia Uganda kwa
usalama wao.
Chanzo: BBCSwahili
No comments:
Post a Comment