Ufaransa na Ujerumani zimetoa wito wa
kufanya makubaliano na Marekani ifikapo mwishoni mwa mwaka huu ili kumaliza
tatizo la ujasusi uliofanywa na Marekani .
Hii inafuatia kuwepo kwa taarifa kuwa
majajusi wa Marekani walikuwa wakifanya udakuzi wa mawasiliano ya simu ya Chansela
wa Ujerumani Angela Merkel pamoja na mamililoni ya raia wa Ufaransa.
Akizungumza katika mkutano wa Jumuiya
ya nchi za ulaya Bi Merkel amesama mbegu ya kutoamiana imepandwa na sasa
itafanya ushirikiano katika mambo ya kiintelejensia kuwa mgumu.
Wakati huo nyaraka mpya za siri
ambazo zimevujishwa na mmarekani Edward Snowden zinaeleza kuwa Marekani imekuwa
ikifanya udakuzi wa simu kwa viongozi wa nchi thelathini na tano duniani.
Waraka huo wa siri uliochapishwa
kwenye gazeti la the Guardian la Uingereza unaeleza Idara ya Ujasusi ya
Marekani ilianza kufuatilia simu hizo baada ya kupewa namba za simu muhimu
zipatazo mia mbili kutoka Idara ya Serikali ya Marekani.
Chanzo: BBCSwahili
No comments:
Post a Comment