Afonso dhlakama wa chama cha Renamo
Ripoti kutoka Musumbiji zinaarifu
kuwa wanaharakati waliojihami kutoka kundi la upinzani la Renamo,wameshambulia
kituo kimoja cha polisi katika mji wa kati wa Maringue.
Kisa hicho kinajiri siku moja baada
ya Renamo kusema kuwa inajiondoa katika mazungumzo ya amani ya mwaka 1992
yaliosababisha kusitishwa kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Renamo ilikaidi makubaliano hayo
baada ya vikosi vya serikali kushambulia kambi iliokuwa na kiongozi wake Afonso
Dhlakana na kumlazimu kutoroka.
Hali ya wasiwasi kati ya serikali na
Renamo imeongezeka katika siku za hivi karibuni huku mapigano yakiripotiwa
katika maeneo mbalimbali.
Inakadiriwa kwamba zaidi ya watu milioni
moja waliuawa katika vita hivyo vya miaka 16 vilivyosababisha mazungumzo ya
amani huku Renamo ikibadilika kutoka kundi la wanamgambo hadi chama cha
kisiasa.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment