Rais wa zimbabwe, Robert Mugabe
ameonya mawaziri wake dhidi ya kuwa na 'nyumba ndogo' akisema kuwa mawaziri hao
wanatumia mali zao nyingi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na wanawake wengi wasio
wake zao.
Mugabe alitoa matamshi hayo wakati wa
harusi ya mpwa wake.
Huku akiwasihi wanandoa kuwa
waaminifu katika ndoa yao, Mugabe alionya dhidi ya kile alichokijata kama tabia
ya wanaume kuwa na 'Nyumba ndogo' nchini Zimbabwe akisema kuwa mawaziri wake
aliowatarajia kuwa watu wenye maadili mema , pia walikuwa na tabia ya
uasherati.
Kwa mujibu wa jarida la New Zimbabwe,
Mugabe alisema kuwa "mali ambayo baadhi ya waziri wanayo ndio chanzo cha
matatizo kwenye ndoa. Nyumba ndogo sio jambo jema na alisema anajua kuwa
mawazri wake wote wana tabia ya uasherati ambalo sio jambo jema katika jamii.''
"nawasihi muachane na tabia hiyo
. Mwanamume mmoja na mke mmoja bila shaka itafanikisha ndoa zenu,'' alisema
Mugabe.
Rais huyo wa muda mrefu ametoa
changamto kwa wanawake kukataa tabia hiyo kwa kutojihusisha na wanaume walio
kwenye ndoa.
"wanawake lazima wapigane dhidi
ya tabia hii mbovu, lakini wao ndio walioko katika nyumba ndogo,'' alisema
Mugabe.
Alisisitiza kuwa usawa wa kijinsia
haupaswi kumaanisha kutupilia mbali tamaduni na maadili.
Mugabe alisema kwa mzaha kuwa japo
hualiakwa kwa harusi nyingi, wakati waume na wake wanapotalikiana, huwa
hajulishwi.
Alisema tabia hii ndio chanzo cha
kuenea kwa ugonjwa wa ukimwi kwani anawafahamu mawaziri wengi wanaougua ugonjwa
huo.
RAIS wa Zimbabwe, Robert Mugabe,
ameonya mawaziri wake dhidi ya kuwa na ‘nyumba ndogo’, akisema kuwa wanatumia
mali zao nyingi katika uhusiano wa kimapenzi na wanawake wengi wasio wake zao.
Alisema tabia hiyo ndiyo chanzo cha
kuenea kwa ugonjwa wa ukimwi, kwani anawafahamu mawaziri wengi wanaougua
ugonjwa huo.
Mugabe ambaye ameiongoza nchi yake
tangu ilipojinyakulia uhuru wake mwaka 1980, alitoa matamshi hayo Jumamosi
iliyopita wakati wa harusi ya mpwa wake.
Huku akiwasihi wanandoa kuwa
waaminifu katika ndoa yao, Rais Mugabe alionya dhidi ya kile alichokitaja kama
tabia ya wanaume kuwa na ‘nyumba ndogo’ nchini Zimbabwe, akisema kuwa mawaziri
wake aliowatarajia kuwa watu wenye maadili mema pia walikuwa na tabia ya
uasherati.
Kwa mujibu wa jarida la New Zimbabwe,
Mugabe alisema kuwa mali waliyonayo baadhi ya waziri ndiyo chanzo cha matatizo
kwenye ndoa. Na kwamba nyumba ndogo si jambo jema katika jamii.
“Nawasihi muachane na tabia hiyo.
Mwanamume mmoja na mke mmoja bila shaka kutafanikisha ndoa zenu,”' alisema
Mugabe.
Mugabe pia alitoa changamto kwa
wanawake kukataa tabia hiyo kwa kutojihusisha na wanaume walio kwenye ndoa.
“Wanawake lazima wapigane dhidi ya
tabia hii mbovu, lakini wao ndio walioko katika nyumba ndogo,” alisema.
Alisisitiza kuwa usawa wa kijinsia
haupaswi kumaanisha kutupilia mbali utamaduni na maadili.
Mugabe alisema kwa mzaha kuwa japo
hualikwa kwenye harusi nyingi, wakati waume na wake wanapotalikiana huwa
hajulishwi.
No comments:
Post a Comment