Thursday, January 1, 2015

KATUNI YA KUFUNGA MWAKA


Wednesday, December 24, 2014

Kesi ya IPTL yapigwa kalenda hadi mwisho wa mwaka


Dar es Salaam. Kesi ya kupinga maazimio ya Bunge iliyokuwa ianze kusikilizwa leo imeahirishwa hadi siku ya kufunga mwaka Desemba 31, 2014.

Wiki iliyopita za kampuni za IPTL na Pan Africa Power Solutions (T) Limited  (PAP) kwa kushirikiana na Harbinder Sighn Sethi zilifungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania kuomba zuio la muda la utekelezaji wa maazimio manane ya Bunge kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow.

Kesi hiyo inayosikilizwa na jopo la majaji watatu ambao ni Augustina Mwarija, Gadi Mjemas na Stella Mugasha jana ilipaswa kuanza kusikilizwa lakini iliahirishwa baada ya mawakili wa upende wa Jamhuri kuomba ahirisho ili waweze kujipanga.

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju aliiomba mahakama hiyo kuiahirisha kesi hiyo kwa madai kuwa wao walichelewa kupata maombi ya kampuni hizo hivyo walishindwa kuyasoma na kujibu.

Hivyo aliiomba mahakama kuiaihirisha kesi hiyo jana  ili waweze kusoma na leo wawasilishe majibu yao na kama upande wa pili na wenyewe utakuwa na cha kujibu  watajibu ili Desemba 31,2014 isikilizwe.


Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo,majaji wanaoisikiliza kesi hiyo walikubaliana na maelezo hayo na kuiahirisha hadi siku hiyo ya Desemba 31,2014.

Chanzo: Mwananchi

Wednesday, April 9, 2014

KATUNI YA LEO NA Chiwambo's Blog


RAIS UHURU KENYATTA ATIMIZA MWAKA MMOJA MADARAKANI

Leo unatimia mwaka mmoja tokea Rais Uhuru Kenyatta aanze kuiongoza Kenya.Katika hotuba yake ya kuingia madaraka Kenyatta alitoa ahadi nyingi. Jee amezitekeleza kwa kiasi gani. Ni mwaka mmoja, tokea Rais Kenyatta aapishwe kuanza kulitumikia taifa la Kenya .

Alitoa ahadi nyingi; ikiwa pamoja na kuuendeleza uchumi, kuuimarisha umoja wa taifa na kuweka utaratibu wa huduma za afya zinazoweza kulipiwa na kila mwananchi .Rais Kenyatta pia aliahidi kuleta uhakika wa chakula, kutenga nafasi za ajira kwa vijana na kugawa "Laptop" kwa watoto wote wa shule za msingi.Lakini aliyoweza kuyafanya ili kuzitekeleza ahadi hizo ni machache hadi sasa.

Bei za vyakula zimezidi kupanda, ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana bado ni wa kiwango cha juu na hasa katika sehemu za mashambani .Aidha mpango wa kugawa "Laptop" kwa watoto wa shule umesahauliwa ndani ya mtoto wa meza kufuatia kashfa.
Mwandishi habari mmoja Inchikirwa Ndelejai amesema serikali ya Kenyatta haijafanya mengi. Amesema serika ya mfungamano wa Jubilee haijafanya ya kutosha. Ameeleza kwamba serikali haikufanya kama ilivyoahidi.

Mwandishsi habari huyo amesema ,ikiwa mtu atawapima wanasiasaa katika msingi wa ahadi walizozitoa, basi kilichofanyika hadi sasa ni cha kusikitisha.

Hatua fulani zapigwa
Hata hivyo hatua kadhaa zimepigwa na serikali ya Kenyatta katika kuzitekeleza baadhi ya ahadi. Mara tu baada ya kuchaguliwa Kenyatta alianza kuutekeleza utaratibu wa kutoa huduma kwa ajili ya wajawazito bila ya malipo.Akina mama hawalipii gharama za kupimwa wanapokuwa wajawazito na pia hawalipii gharama za kujifungua.Katika hotuba yake Rais Kenyatta ,alisifu mafanikio yaliyopatikana katika uchumi na hatua zilizochukuliwa katika kupambana na ufisadi.

Hatua fupi katika kupambana na ufisadi
Hata hivyo kuhusu ufisadi ndani ya polisi,mwakilishi wa Wakfu Ujerumani wa " Heinrich Böll" nchini Kenya Katrin Seidel amesema kwamba maafisa wengi wa polisi waliohusika na vitendo vya ufisadi vilivyoweza kuthibitishwa bado wanaendelea na kazi na bado wamo katika ngazi za uongozi pia katika idara ya usalama. Mwakilishi huyo wa Wakfu wa Ujerumani ,bibi Seidel amesema watu wengi nchini Kenya wanahisi kwamba hawahudumiwi kwa kiwango cha kutosha katika suala la usalama.

Kutokana na shambulio la magaidi kwenye jengo la maduka,Westgate mjini Nairobi mwezi Septemba mwaka uliopita Wakenya wengi wamepoteza imani juu ya idara za usalama. Lakini juu ya suala la usalama Rais Uhuru Kenyatta amesema " usalama wa watu wetu na ulinzi wa mipaka ya nchi ni miongomi mwa wajibu wangu mkuu." Rais Kenyatta amesema vitisho vyovyote dhidi ya mipaka ya Kenya vitakabiliwa kwa uwezo na nguvu zote za watu wa Kenya.

Umaarufu wa Kenyatta katika utaifa
Katika upande mwingine Rais Kenyatta anatumia turufu ya utaifa ili kuhakikisha umaarufu wake. Hata kesi inayomkabili kwenye Mahakama Kuu ya Kimataifa ya ICC inapalilia umaarufu wake.

Rais Kenyatta anakabiliwa mashkata ya uhalifu dhidi ya binadamu. Katika ghasia zilizotokea nchini Kenya kufuatia uchaguzi wa Rais mnamo mwaka wa 2007 inadaiwa kuwa Kenyatta ambae wakati huo alikuwa kiongozi wa chama ndiye aliehamamisha makundi yaliyowatimua watu wa makabila mengine,yaliyofanya ubakaji na kuwaandama watu wa jamii nyingine.
Mwandishi:Fischer ,Hilke,
Tafisiri:Mtullya Abdu.
Mhariri:Yusuf Saumu

DW.DE

SHANGAZI WA RAIS OBAMA AFARIKI DUNIA.

Shangazi wa rais Obama  Zeituni  Onyango ambaye  kwa wakati fulani alinyimwa hifadhi hapa Marekani lakini akaendelea kuishi kinyume cha sheria kwa miaka kadhaa katika jimbo la Masachussets  amefariki  dunia akiwa na umri wa miaka 61.

Wakili wa masuala ya Uhamiaji wa  Onyango amesema amefariki katika hospitali moja baada ya kuugua ugonjwa saratani na matatizo ya kupumua . Aliugua tangu mwezi January.
Onyango alihamia Marekani kutoka Kenya mwaka 2000 na alinyimwa hifadhi ya kisiasa na jaji wa Uhamiaji mwaka 2004. Hakuondoka nchini na aliendelea kuishi kwenye nyumba za umma huko Boston. Hali yake ya ukaazi wa Marekani  ilitangazwa hadharani  siku chache kabla ya Bw.Obama kuchaguliwa rais Novemba 2008.


Chanzo: VOA

UKRAINE WARNS PRO-RUSSIAN SEPARATISTS


Authorities say they are prepared to use force to clear buildings occupied by pro-Russian separatists in country's east. Ukrainian authorities have warned they are prepared to use force to clear several government buildings seized by pro-Russian separatists in the east of the country.

Wednesday's warning came as protesters continued to occupy the headquarters of Ukraine's Security Service in the eastern city of Luhansk.

Hundreds of supporters camped outside and shouting "Putin! Putin!" in support of the Russian President, the Associated Press news agency reported.

Arsen Avakov, the Ukrainian interior minister, said the standoff in Luhansk and the two neighbouring Russian-leaning regions of Donetsk and Kharkiv must be resolved within the next two days.

"I want to repeat that there are two options: political settlement through negotiations and the use of force," Avakov told reporters. "We are ready for both options."

Avakov was speaking as anti-government protesters in Luhansk erected high barricades along a thoroughfare running in front of the security service premises.

The Security Service had earlier said that the separatists inside the building, armed with explosives and other weapons, allowed 56 hostages to leave the building during the night. A spokeswoman said there were no other hostages.

But Tetyana Pohukay, a regional police spokeswoman, disputed that statement, saying there had never been any hostages inside, according to the Interfax news agency.

The Luhansk security services building was among several government offices seized by pro-Moscow groups on Sunday in an escalation of protests against the interim government in power since President Viktor Yanukovich was forced to quit in February after months of protests against his decision to ditch an EU trade pact in favour of closer ties with Moscow.

Peaceful solution

Serhiy Tyhipko, a lawmaker associated with the previous Ukraine government, urged the authorities not to storm the building in Luhansk, calling for a negotiated peaceful solution.

Tyhipko said the protesters were demanding to turn Ukraine into a federal state with broad regional autonomy, not to secede.

"The people are not bringing up the issue of breaking off from Ukraine and are not calling for the help of foreign countries,'' Tyhipko said on his Facebook page.

Turning Ukraine into a federation is Russia's key demand and the new government in Kiev has refused to fulfill it, calling it a precursor to a break-up.

In Donetsk, where protesters were still occupying the government building, the regional governor was meeting with key figures in the pro-Russian protest movement to try to find a solution to the crisis.

"The ultimatum made put the pressure on people here in Donetsk," Al Jazeera's Kim Vinnell said, reporting from the eastern region.

She added that negotiations were under way between both separitists and police in Donetsk and Luhansk.

"Now, with this ultimatum, it will be a question of what kind of deal can both sides come to. Both protesters and police are very keen to avoid any bloodshed," she said.

All the cities affected by the uprisings are in Ukraine's industrial Russian-speaking heartland in the east, which has a large population of ethnic Russians and where economic and cultural ties to Russia are strong, according to AP.

Many residents are suspicious of the government that took power in February.

Overnight, speakers at a gathering in front of the building condemned the government in Kiev and renewed demands to be allowed to hold a referendum on declaring autonomy for their region.

That demand is similar to one that preceded Crimea's annexation by Russia.


Source: Al Jazeera And AP

Hofu yatanda malumbano makali kuibuka kesho

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa,Peter Kuga Mziray.
Mwenyekiti  wa Baraza la Vyama  vya Siasa, Peter Kuga Mziray, ameonyesha wasiwasi wake kwamba huenda mvutano mkubwa ukazuka bungeni kesho na Ijumaa wakati kamati 12 za Bunge Maalum la Katiba zitakapowasilisha taarifa bungeni baada ya kupitia na kuchambua sura mbili za Rasimu ya Katiba, ya kwanza na ya sita.

Sura ya kwanza inazungumzia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alama na Sikukuu za Taifa, Lugha za Taifa na lugha za alama na Tunu za Taifa.

Sura ya sita inazungumzia muundo wa Muungano, vyombo vya utendaji vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mamlaka ya serikali ya Muungano, mambo ya Muungano, nchi washirika, mamlaka ya nchi washirika, mahusiano kati ya nchi washirika, mawaziri wakaazi, mamlaka ya wananchi na wajibu wa kulinda Muungano.

Akizungumza na NIPASHE jana, Mziray alisema mambo yalikwenda vizuri katika vikao vya kamati, lakini kujadili sura hizo mbili ndani ya bunge zima mabishano yataanza.

“Hizo sura mbili ndizo zinaleta ugumu, ndipo kwenyewe,” alisema Mziray ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge hilo na kuongeza: “Hali bado siyo nyepesi, bado sura hizo ndizo ngumu na ndizo zinaleta mambo.”

Aprili Mosi, mwaka huu kamati 12 za Bunge hilo zilitawanyika katika maeneo manne kwa ajili ya kuchambua na kujadili sura ya kwanza na ya sita ambazo ndizo zenye mvutano mkali.

Miongoni mwa mambo ambayo yalizua utata katika Sura ya Kwanza ni ibara 1(1)  inayosema  Tanzania ni nchi na Shirikisho lenye mamlaka kamili ambalo limetokana Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla ya Hati ya Makubalino ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi huru.

Katika ibara hiyo wajumbe kadhaa walitaka neno shirikisho ilitoke badala yake iwe Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi yenye mamlaka kamili.

Hali hiyo ilisababisha baadhi ya kamati kukosa theluthi mbili ya kura kutoka katika kila upande wa muungano ambazo zinatakiwa kwa mujibu kanuni 64 (1).

Eneo lingine lililozua mvutano ni Ibara  1(3) inayosema Hati ya Makubaliano ya Muungano iliyorejewa katika Ibara ndogo ya kwanza ndiyo msingi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba hii kwa kadri itakavyorekebishwa, itakuwa ni muendelezo wa makubaliano hayo.

Kutokana na hali hiyo, wajumbe kadhaa walitaka ufafanuzi kuhusu Hati ya Muungano na kutaka kuiona.

Hali hiyo ilisababisha kamati Na 2 na 8 kumuita aliyekuwa Katibu wa Bunge wakati wa Muungano, Pius Msekwa, kwenda kutoa maelezo. Hata hivyo, suala hilo bado halijapata ufumbuzi hususani mahali ilipo hati hiyo na madai ya utata wa saini.

Katika hatua nyingine, Mziray alisema kuwa baraza lake liliandaa mkutano wa dharura wa viongozi wa vyama vya  siasa kwa ajili ya kupata mwafaka na kuwekana sawa kufuatia matukio kadhaa ya mivutano katika Bunge Maalumu la Katiba Jumatatu iliyopita, lakini uliahirishwa kutokana na uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Chalinze na Siku ya Kumbukumbu ya Karume.

Alisema siku inayoweza kupangwa ni Jumapili ambayo ni rahisi kuwapata viongozi wengi kwa kuwa hakuna vikao vya Bunge.

Naye Katibu wa Baraza hilo, Jaji Francis Mutungi, aliiambia NIPASHE kuwa wanauandaa tena mkutano huo ili ufanyike kati ya Aprili 22 na mwisho wa mwezi.

Jaji Mutungi ambaye pia ni Msajili wa Vyama vya Siasa, alisema watawawaalika watu wengine wakiwamo viongozi wa dini na kwamba kabla ya mkutano huo, atakutana na baadhi ya makatibu wakuu wa vyama vya siasa.


CHANZO: NIPASHE

Uganda yatuma ujumbe polisi wake kuvamia Tanzania

Ujumbe  wa askari wa Jeshi la Polisi la Uganda umewasili nchini kwa kile kinachodaiwa kuja kufanya mazungumzo ili kupata maridhiano kufuatia kitendo cha askari wake wakiwa na bunduki kuvamia eneo la Mutukula, mkoani Kagera, na kurusha risasi ovyo zilizojeruhi Watanzania wawili.

Habari zilizopatikana jana zinaeleza kuwa askari hao ujumbe wa askari hao umewasili nchini wakiongozwa na mmoja wa viongozi wakuu wa Jeshi la Polisi Mbarara, nchini humo.

NIPASHE, ambayo ilifika katika Kituo Kikuu cha Polisi jana asubuhi iliwashuhudia askari wanne wa Uganda waliovalia sare, wakiwa nje ya kituo hicho, ambako mwenzao mmoja anashikiliwa kwa tuhuma hizo.

Hata hivyo, habari nyingine zilieleza kuwa mbali na kuja kutafuta maridhiano baina yao na wenzao wa Tanzania, ujumbe huo pia umekuja nchini kwa ajili ya kumchukulia dhamana mwenzao anayeshikiliwa na polisi wa Tanzania.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, George Mayunga, alipotakiwa jana kuelezea suala hilo, alisema hadi jana alikuwa hajapata kibali cha kuzungumzia suala hilo kutoka Makao Makuu ya Polisi, jijini Dar es Salaam.

Msemaji wa Jeshi hilo nchini, Advera Senso, jana hakupatikana kuzungumzia kinachoendelea kuhusiana na kadhia hiyo na hata alipopigiwa simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

Hata hivyo, juzi alikaririwa akisema kinachopfanywa na Jeshi la Polisi ni kuchunguza ili kujua sababu za askari hao kuendesha operesheni hiyo nchini bila kuwaarifu wenzao wa Tanzania kama sera ya Interpol (Polisi wa Kimataifa) inavyotaka.

Askari saba kutoka Uganda Jumamosi wiki iliyopita wakiwa na silaha hizo, walivamia eneo hilo kwa kile kilichodaiwa kuwa walikuwa wakiwatafuta watuhumiwa wa wizi wa pikipiki waliokimbilia Tanzania.

Chanzo: Nipashe

Necta kuongeza kiwango cha ufaulu sekondari

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Jenista Mhagama.

Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), limejipanga kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa sekondari nchini kwa kusambaza vitabu vya tathimini ya uchambuzi wa ufaulu kwa kila mtihani uliofanywa.

Usambazaji wa vitabu hivyo utakafanyika kwa shule zote nchini ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa sasa (BRN) ili kuwawezesha walimu na wanafunzi kubaini makosa kwenye mitihani mbalimbali iliyofanywa.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenista Mhagama, akizindua vitabu hivyo mwishoni mwa wiki  iliyopita jijini Dar es Salaam, alisema vitaonyesha tathimini ya ufaulu kwa kila swali katika kila somo, matakwa ya maswali na jinsi watahiniwa walivyoyajibu kwa kupata au kukosa.

“Uchambuzi huu utawasaidia walimu  na wanafunzi kubaini makosa mbalimbali yanayofanywa na watahiniwa wakati wa kujibu maswali na hivyo kujifunza mbinu bora za kujibu maswali hayo, itasaidia kuboresha kiwango cha ufaulu cha watahiniwa kwa miaka ijayo,” alisema.

Alisema ni vema vitabu hivyo vikawekwa kwenye tovuti ili wadau wengi waweze kuvisoma kwa njia ya mtandao na kupata taarifa sahihi ya tathimini ya ubora wa elimu na hivyo kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuboresha kiwango cha elimu.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde, alisema jitihada za pamoja katika kuboresha ufundishaji na ujifunzaji zinahitajika ili kuongeza ubora wa elimu kwenye masomo yote kwa kuwa ufaulu kwenye masomo yote uko chini ya asilimia 50.

Alisema chini ya BRN, Wizara ilijiwekea mikakati tisa ya kutekeleza ambayo ni upangaji wa shule kwa ubora wa matokeo, utoaji wa tuzo kwa shule zilizofanya vizuri, kuwa na kiongozi cha usimamizi wa shule, upimaji wa kitaifa wa stadi za kusoma.

Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) (Elimu), Kassim Majaliwa, alisema vitabu hivyo vitawasaidia walimu na wanafunzi kubainia mambo yenye changamoto katika ujifunzaji na ufundishaji na sababu za kuwafanya watahiniwa washindwe kujibu maswali.

Majaliwa aliwaagiza maafisa elimu wa mikoa, wilaya na kata kufuatilia matumizi ya vitabu hivyo na kuhakikisha kila shule inapata nakala  kwa kuwa ni nyenzo muhimu katika kufanya kazi.


CHANZO: NIPASHE

Watu wenye ulemavu watengewe bajeti`

`

Diwani wa Kata ya Ngarenaro, Isaya Doita, (Chadema), amezitaka halmashauri kutenga bajeti kwa ajili ya watu wenye ulemavu  kupata mahitaji yao badala ya halmashauri hizo kutenga asilimia 10 kwa ajili ya wanawake na vijana pekee.

Aidha, watoto wenye ulemavu wa kutosikia, wameiomba jamii kuachana na tabia ya kuwaficha majumbani badala yake wawapeleke mashuleni kwa ajili ya kupata elimu na kujikomboa kimaisha.

Akizungumza na watoto wenye ulemavu pamoja na wananchi mbalimbali waliokusanyika kuwasikiliza   viwanja vya Soko Kuu jijini Arusha.

Alisema wakati umefika sasa kila kata kutambua watu wenye ulemavu ili waweze kutengewa  bajeti yao na kupata misaada mbalimbali waweze kuinuka badala ya kuonekana ni mzigo ndani ya familia zao.

Alisema ikiwa halmashauri inatenga asilimia 10 yaani asilimia 5 inakwenda kwa kinamama na tano inakwenda kwa vijana huku jamii yenye ulemavu ikiwa haitengewi bajeti .

Naye mwakilishi wa kutetea haki za watoto pamoja na watoto wenye ulemavu mkoani Arusha, Hafsa Mgaza, aliiomba jamii kuacha tabia ya kunyanyasa watoto hususan wenye ulemavu kwani kila mtu ni mlemavu mtarajiwa bali walindwe na kuheshimiwa kama jamii nyingine zenye mahitaji.

Pia alisisitiza kuwa si jambo jema kumuona mlemavu akinyanyasika na mwenye viungo akimwangalia.

Aidha, aliiomba serikali pamoja na taasisi mbalimbali kuhakikisha wanapojenga majengo yanakuwa ni rafiki kwa jamii hiyo hususan vyooni kwani baadhi yao hupata taabu wanapohitaji kwenda msalani na maeneo mbalimbali kwa ajili ya mahitaji yao.

Ofisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Arusha, Blandina Mkini, alisema serikali itaendelea kushirikiana na jamii hiyo katika kuhakikisha haki zao zinalindwa na kutoa rai kwa jamii kuacha tabia ya kuwabaka watu wenye ulemavu.

CHANZO: NIPASHE

Kerry says Russia stirs 'chaos' in Ukraine

President Obama

US secretary of state says Russia sent "agents" to destabilise Ukraine, as pro-Russians seize offices in eastern cities. The US secretary of state, John Kerry, has bluntly blamed Russia of "unmistakable involvement in destabilising" Ukraine by sending "agents" to its eastern cities.

Kerry on told US Congress on Tuesday that the Kremlin was seeking to "create chaos" in Donetsk, Kharkiv and Luhansk as a pretext for more military intervention. "Everything that we've seen in the last 48 hours, from Russian provocateurs and agents operating in eastern Ukraine, tells us that they've been sent there determined to create chaos," Kerry said, adding that he would next week meet his Russian counterpart, Sergei Lavrov, to discuss the crisis.

Shortly after Kerry's comments, Ukraine's SBU state security service said pro-Russian activists had placed explosives in a seized government office in Luhansk, and were holding about 60 people hostage.

"These actions are extremely dangerous and endanger the lives of people both inside and outside of the building. They are using terrorist measures," and SBU statement said.

Luhansk pro-Russian protesters quickly denied the claims.

"There are no explosives, no hostages. We do not need hostages to get what we want," said Anton, one of the protesters who described himself as a coordinator of the action.

In recent days pro-Russian activists seized government buildings in several cities in Ukraine's east, declaring independence and vowing to vote on splitting from Ukraine.

Ukrainian police cleared protesters from a regional administration building in Kharkiv in a lightning nighttime operation on Monday, but others held out in the eastern cities Luhansk and Donetsk.

Russian efforts

Lavrov and Catherine Ashton, the European Union foreign policy chief, on Tuesday discussed possible international efforts to find a solution to the Ukraine crisis, the Russian foreign ministery said in a statement.

In a telephone conversation initiated by Ashton, Lavrov reaffirmed Russia's proposal for "an authentic Ukraine-wide dialogue involving all political forces and regions" aimed at reaching agreement on constitutional reforms, the statement said.

Russia has long been suggesting "federalisation" of Ukraine in order to give more autonomy to the regions of the country, claiming it would make sure ethnic Russian population were not marginalised by Kiev's central government.

Ukrainian government sees the Russian plan as an effort to break up the country.


Source: Reuters

Matapeli wajipenyeza TCRA

MAMLAKA ya Mawasiliano imebaini kuwa uwepo wa mtandao wa matapeli wanaotumia jina la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kutumia tovuti iitwayo “TCRA Foundation”, inayodanganya kutoa mikopo kwa maendeleo kwa watu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Prof. John Nkoma, tovuti inayotumika ni http://tcra-foundation.wix.com/tcrafoundation.

Alisema mtandao huu umetengenezwa kwa kutumia picha zilizopo kwenye mitandao mbalimbali  zikiwaonyesha Rais Jakaya Kikwete, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makawe Mbarawa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Prof. John Nkoma.

Aidha mtandao huu unadai kuwa mamlaka kwa kushirikiana na kampuni za simu za Vodacom na Tigo pamoja na Benki ya CRDB na NMB zinashirikiana kuendesha foundation hiyo.

“Mamlaka ya Mawasiliano inawatahadharisha wananchi kuwa haina “Foundation” yoyote ya kutoa misaada ya fedha. Mtandao huu unatumika kuwalaghai wananchi na kuwaibia fedha zao kwa kuwataka watume fedha za kujiunga na mtandao huo kwa namba za simu za Tigo na Vodacom zinazoonyesha kusajiliwa kwa jina la Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania. Sio kweli na ni wizi na udanganyifu,” alisema.

Prof. Nkoma alisema Mamlaka ya Mawasiliano inawataka wananchi kuwa na tahadhari na watu hawa ambao hutumia mitandao ya mawasiliano ya simu na intaneti kufanya utapeli kwa kutotuma fedha wala kujiunga na mitandao ya namna hiyo.

Chanzo: Tanzania Daima

Mnyika ashupalia sheria ya kuzuia bodaboda

MADEREVA wa pikipiki (bodaboda) jijini Dar es Salaam wamelalamikia kitendo cha Jeshi la Polisi kuwazuia kuingia ndani ya kivuko cha Kigamboni kwa madai ya kuziondoa pikipiki hizo katikati ya jiji.

Wakizungumza kwa jazba jana asubuhi baada ya kuzuiliwa kuingia kwenye pantoni kutoka Kigamboni kwenda Feri, baadhi ya madereva hao walisema hawajatendewa haki kwa kuwa sio wote wanaofanya biashara ya kupakiza abiria, wengine wanazitumia kwa usafiri binafsi.

Bakari Musa, mmoja wa madereva hao, alisema jeshi hilo halikuwapa taarifa ya zuio la wao kuvuka na pikipiki zao hadi watakapokuwa na kibali maalumu.

Alisema kitendo kilichofanywa leo si cha kiungwana kwani kimesababisha wengi wao kuchelewa kazini baada ya kufika Kivukoni na kuzuiwa.

Wakati madereva hao wakilalamikia usumbufu huo, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick ameudanganya umma kwamba Bunge lilitunga sheria ya kuzuia bodaboda na bajaj kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

“Si kweli kwamba kuna sheria ilipitishwa Machi 12, 2010 kama ilivyoelezwa na mkuu huyo wa mkoa, badala yake tarehe hiyo ni siku ambayo aliyekuwa Waziri wa Miundombinu Dk. Shukuru Kawambwa alitunga kanuni.

“Hata hivyo, kanuni hizo nazo hazikupiga marufuku bodaboda na bajaj kuingia katikati ya jiji bali zilikasimu mamlaka kwa halmashauri za Serikali ya Mitaa kuweka utaratibu wa namna vyombo hivyo vya usafiri vitakavyoingia mjini,” alisema Mnyika.

Alisema kwa kuzingatia maelezo hayo, alimtaka mkuu wa mkoa asitishe agizo lake na halmashauri za jiji hilo ziweke utaratibu kwa mujibu wa kanuni na kuzingatia malengo ya kulinda usalama, kupunguza foleni, kuhakikisha fursa za ajira kwa vijana na usafiri wa gharama nafuu kwa wananchi.

Kwa mujibu wa Mnyika, sheria ya Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) haikutungwa mwaka 2010 bali ilitungwa mwaka 2001 huku akisisitiza kwamba mwaka 2010 zilitungwa kanuni za Transport Licensing (Motor Cycles and Tricycles) zilizochapwa kwenye gazeti la serikali namba 144 la Aprili 2 mwaka huo.

Hivi karibuni Jeshi la Polisi, Sumatra na viongozi wa madereva, waliwataka madereva wa pikipiki kuendelea kutii amri ya kutoingia mjini kwa pikipiki za miguu miwili (bodaboda) na mitatu (bajaj).

Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa operesheni ya kuzuia vyombo hivyo kuingia katikati ya jiji ni endelevu.

“Tutaendelea na operesheni hii, lengo si kuwakomoa bali ni sheria zipo wazi na lazima zifuatwe,” alisema na kuongeza kuwa wanazuia pia kutokana na uhalifu wa kutumia pikipiki uliokithiri hasa maeneo ya katikati ya jiji.


Chanzo: Tanzania Daima

WHO: uvumi wa maambukizi ya Ebola ukome

Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema kuwa kuzuka kwa Homa ya Ebola Magharibi mwa Afrika ni mojawapo ya changamoto kubwa zaidi ambazo limewahi kukabiliana nayo.

Shirika hilo limesema kuwa italichukua hadi miezi minne kuthibiti ugonjwa huo. Wakati huohuo shirika la kutoa misaada ya matibabu ya bure, Medicins Sans Frontieres, limesema kuwa linaendelea kufanya mashauriano na viongozi wa kijamii katika Wilaya moja Kusini mwa Guinea, ambalo lilisimamisha shughuli zake baada ya vituo vyake kadhaa kushambuliwa na wakaazi wa eneo hilo.

Msemaji wa shirika hilo katika mji mkuu wa Guinea wa Conakry - Sam Taylor - amesema inaeleweka kwamba watu wana uoga mkubwa.
"Sio taharuki, kimsingi huu ni uoga. Na tunaelewa hilo. Ni ugonjwa wa kugovya na pia ni mpya nchini Guinea, na kuna uvumi unaosambaa na pia kuna habari za kuotosha zinazoenea; na tunachohitaji kuona kwa wingi sasa ni watu kwenda kwa jamii mbalimbali kueleza ugonjwa huu, jinsi unavyoenea, na jinsi usivyoenea," alisema Bwana Taylor.

Ugonjwa huo umewaua watu 111 katika nchi za Guinea na Liberia tangu uchipuke mwezi uliopita.

MAGAZETINI LEO JUMATANO 09-04-2014 NA Chiwambo's Blog