Baadhi
ya wabunge , wameitupia lawama Serikali baada ya kutoridhishwa na majibu
wanayopewa juu ya hatua mbalimbali zilizochukuliwa kukomesha vitendo vya
ujangili wa wanyama jambo linaloweza kuua sekta ya utalii nchini.
Hali
hiyo ilijitokeza bungeni Mjini Dodoma jana wakati wa kipindi cha maswali na
majibu ambapo baadhi ya wabunge walitaka Serikali itoe taarifa sahihi za ukubwa
wa tatizo hilo na kuwataja wahusika badala ya kunyamaza.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Bw. William Lukuvi,
alisimama na kutoa ufafanuzi wa kina juu ya hatua mbalimbali ambazo Serikali
imezichukua kukabiliana na biashara haramu ya meno ya tembo.
Alisema
tayari imeundwa timu inayofanya Operesheni Maalumu ya kupambana na kuwabaini
wahusika wa biashara hiyo hivyo ni mapema sana kuwataja kwa sasa.
"Watu
wanaotuhumiwa ni wengi, hata msaidizi wangu jimboni alikamatwa akiwa ofisini na
kupigwa akihusishwa na biashara hiyo ila baadaye walimuachia baada ya
kujiridhisha.
Kwa
upande wake, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Bw. Shamsi Vuai
Nahodha, alisema suala la ujangili si la kufanyiwa mzaha kutokana na athari
zake kuwa kubwa.
"Hapa
hakuna kulindana, mtu yeyote ambaye itabainika anahusika na biashara ya meno ya
tembo, tutamkamata na kumchukulia hatua za kisheria," alisema Bw. Nahodha.
Aliwataka
wanasiasa kutoingilia suala hilo kwani zipo taarifa za baadhi yao kutumia nguvu
ya siasa ili kuwatetea wahalifu kwani Serikali haina mzaha na jambo hilo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, Bw. James Lembeli, alidai
kuwa wapo baadhi ya makamanda walioko maeneo mbalimbali ya nchi ambao
wanajihusisha na vitendo vya ujangili.
Aliitaka
Serikali itoe ufafanuzi kwanini inashindwa kuwachukulia hatua za kisheria
badala yake wanaendelea kuwafumbia macho.
Wakati
huo huo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Bw. Lazaro Nyalandu, alisema hadi
sasa wapo maofisa wa vyombo vya usalama wanashikiliwa polisi kwa tuhuma za
ujangili.
Bw.
Nyalandu aliyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigamboni, Dar es
Salaam, Bw. Faustin Ndungulile juu ya hatua zilizochukuliwa na Serikali
kudhibiti janga hilo nchini.
Alisema
Serikali haitawavumilia makamanda na wanasiasa wanaojihusisha na vitendo vya
ujangili hasa mauaji ya tembo ambapo Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazotisha
kwa biashara haramu ya meno yake.
"Hali
hii inachangiwa na Serikali kuwa na uhaba wa askari wanyamapori anayepaswa
kulinda umbali wa kilomita 25 tofauti na zamani alikuwa akilinda kilomita za
mraba 150,000.
"Serikali
ina mpango wa kuyatenga maeneo yanayofaa kuwa vitaru kutokana na malalamiko
yaliyopo kuwa vinatumika kuwindia tembo kitendo ambacho ni kinyume cha
sheria," alisema.
Awali
Mbunge wa Arusha Mjini, Bw. Godbless Lema, alidai waliopewa vitalu pembezoni
mwa hifadhi za wanyama huvitumia kuwaua wanyama ambao wanakatazwa kuwindwa
kisheria
No comments:
Post a Comment