Kwa waziri mkuu wa Uingereza tofauti baina ya mema na mabaya
ipo wazi kabisa mithili ya usiku na mchana. Mashirika ya ujasusi yanapambana na
magaidi na anaetoa habari zozote juu ya kazi za mashirika hayo ni adui.
Mwandishi wetu Regina Menning anasema
katika taarifa yake kwamba Uingereza inaelekea katika mkondo wa kuubana uhuru
wa vyombo vya habari kwa kisingizio cha kuulinda usalama wa taifa.
Waziri Mkuu wa Uingereza David
Cameron aliufafanua msimamo huo kandoni mwa mkutano wa kilele wa viongozi wa
nchi za Umoja wa Ulaya uliofanyika mjini Brussels hivi karibuni. Alipozumzia
juu ya adui, Waziri Mkuu Cameron alikuwa na maana ya Edward Snowden wakala wa
zamani wa shirika la ujasusi la Marekani ka NSA aliefichua siri za shirika
hilo. Kwa Waziri Mkuu wa Uingereza Cameron vyombo vya habari, kama gazeti la
"Guardian "pia ni adui wa harakati za kupambana na ugaidi .
Mwandishi wa gazeti hilo Glenn Greenwald
alizichapisha habari za kwanza za siri alizopewa na aliekuwa mfanyakazi wa
shirika la ujasusi la Marekani la NSA, Edward Snowden. Waziri Mkuu wa Uingereza
ametoa vitisho dhidi ya gazeti la "Guardian" Na siyo yeye peke yake.
Kwa muda wa wiki kadhaa sasa vyombo
vya habari muhimu nchini Ungereza vimekuwa vinalisakama gazeti la Guardian.
Vyombo hiyvo vinesema katika tahariri kali kwamba kwa kukubali kuzichapisha
siri zilizofichuliwa na Edward Snowden, gazeti hilo limewasaida maadui wa
Uingereza. Kiongozi wa maripota wasiojali mipaka tawi la Ujerumani Michael
Rediske amesema vitisho kama hivyo ni jambo lisilowezekana nchini
Ujerumani.Amekumbusha juu ya mzigo wa historia unaobebwa na wajerumani.
Nchini Ujerumani watu wanakumbuka
yaliyotokea wakati wa utawala wa mafashisti.Dhana kama maslahi ya kitaifa au
siri za nchi zilitumika kama sababu. Katika baadhi ya nchi, miongoni mwao
,Uingereza vitabu vya sheria vinatumiwa kuimarisha ulinzi wa siri za
nchi."
Mkuu huyo wa waandishi wa tawi la
Ujerumani la waandishi wa habari wasiojali mipaka bwana Rediske amesema vyombo
vya habari nchini Ujerumani vina makucha ya kuwaewzesha kujitetea.Ametoa mfano
wa alieyekuwa Rais wa Ujerumani, Christian Wulff aliejaribu kumtisha mhariri
mkuu wa gazeti la "Bild.
Rais huyo wa zamani alimpigia simu
mhariri huyo ili kujaribu kuzuia kuchapishwa kwa taarifa juu ya mkopo uliokuwa
na utata aliopewa bwana Wulff. Mkasa huo ulitifua tufani iliyomng'oa madarakani
Rais huyo. Lakini serikali ya Uingereza inavishinikiza vyombo vya habari kwa
kisingizio cha usalama wa taifa. Hata hivyo mwakilishi wa waandishi habari
wasiojali mipaka bwana Rediske amesema inapasa kutilia maanani kwamba magaidi
waliwahi kufanya mashambulio mabaya katika treni ya chini ya ardhi nchini
Uingereza.
Mwandishi:Menning, Regina
Tafsiri:Mtullya Abdu
Mhariri: Yusuf Saumu
Chanzo:
DWswahili
No comments:
Post a Comment