Waasi wa kundi la M23.
Mapiganao yameibuka upya kati ya wanajeshi wa serikali na
waasi kaskazini-mashariki mwa Kongo, zimesema pande mbili na Umoja wa Mataifa,
siku chache baada ya kushindwa kwa ya mazungumzo ya amani mjini Kampala.
Msemaji wa waasi wa M23 Vianney
kazarama alisema mapigano hayo ambayo yaliwalaazimu maelfu ya raia kuyakimbia
makaazi yao, yalitokea umbali wa kilomita 25 kaskazini mwa Goma, mji muhimu wa
wakaazi milioni moja uliyopo katika eneo lenye utajiri mkubwa wa madini la
mashariki, lakini linalokabiliwa na machafuko ya mara kwa mara.
Rwanda yatishia kujibu mapigo
Nchi jirani ya Rwanda iliwashtumu wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwa kurusha makombora matatu ndani ya mipaka yake na kutishia kujibu iwapo mashambulizi yataendelea. Kazarama alisemam jeshi lilishambulia ngome za waasi mapema siku ya Ijumaa, lakini jeshi hilo lilisitiza kuwa lilishambuliwa kwanza -- madai yanayoungwa mkono na duru kutoka ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO.
Nchi jirani ya Rwanda iliwashtumu wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwa kurusha makombora matatu ndani ya mipaka yake na kutishia kujibu iwapo mashambulizi yataendelea. Kazarama alisemam jeshi lilishambulia ngome za waasi mapema siku ya Ijumaa, lakini jeshi hilo lilisitiza kuwa lilishambuliwa kwanza -- madai yanayoungwa mkono na duru kutoka ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO.
Taarifa ya MONUSCO, ambayo ilishiriki
mapigano hayo sambamba na jeshi la Kongo, ilisema ghasia ziliendelea kwa siku
nzima. MONUSCO ilisema ilikuwa na wasiwasi mkubw ajuu ya kuanza tena kwa uadui,
na kuwatolea wito waasi wa M23 kurudi kwenye meza ya mazungumzo. "Niko
makini katika juhudi zetu za kuwalinda raia na kuyatangua makundi yote yenye
silaha ili kurejesha amani na utulivu," alisema mkuu wa MONUSCO martin
Kobler.
Mkuu wa MONUSCO, Martin Kobler.
Mwanaharakati wa haki za binaadamu
katika eneo hilo aliziona helikopta za Umoja wa Mataifa zikiruka juu ya kijiji
cha Kibumba, ambacho ni ngome ya M23 iliyoshambuliwa, na alisema kuwa raia
walikuwa wanakimbia kuelekea mpaka wa Rwanda.
Baraza ya usalama la Umoja wa Mataifa
mwezi Machi liliidhinisha kupelekwa kwa kikosi maalumu cha Afrika chenye
wanajeshi 3,000 chini ya MONUSCO, ambacho kinaongozwa na Jenerali kutoka
Tanzania, kikiwa na mamlaka ya kufanya mashambulizi dhidi ya makundi ya waasi
nchini Kongo.
Jeshi la Rwanda lilisema kuwa makombora
matatu yaliangukia katika ardhi yake, na kumjeruhi raia. "Kama hawako
tayari kusitisha hili, tutajibu mara moja na itauma," alisema balozi w
arwanda katika Umoja wa Mataifa Eugene Richard Gasana baada ya mazungumzo ya
baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusiana na wasiwasi uliyoongezeka.
Wizara ya wakimbizi ya Rwanda ilisema kati ya watu 2,500 na 3,000 wamekimbilia
nchini humo kupitia mipaka miwili.
Hujuma dhidi ya mazungumzo ya amani
Siku ya Jumatatu, makundi hasimu yalitangaza kuwa yanasitisha mazungumzo ya amani yanayofanyika katika mji mkuu wa Uganda Kampala, licha ya shinikizo kutoka kwa Umoja wa Mataifa kukomesha uasi huo wa miaka miwili na nusu unaosababisha uharibufu mkubwa mashariki mwa Kongo.
Siku ya Jumatatu, makundi hasimu yalitangaza kuwa yanasitisha mazungumzo ya amani yanayofanyika katika mji mkuu wa Uganda Kampala, licha ya shinikizo kutoka kwa Umoja wa Mataifa kukomesha uasi huo wa miaka miwili na nusu unaosababisha uharibufu mkubwa mashariki mwa Kongo.
Kwa mujibu wa serikali ya Kongo,
mazungumzo hayo yalisitishwa kutoka na tofauti ju ya msamaha kwa wanajeshi
walioasi na kurejeshwa kwao katika jeshi la taifa. Ikiungwa mkono na jamii ya
kimataifa, serikali ya Kongo inakataa kutoa msamaha kwa karibu viongozi 80 wa
kundi la M23, na kuwarejesha tena katika vyeo vya kijeshi.
Rais Joseph Kabila wa Kongo, na Paul
Kagame wa Rwanda.
Katika taarifa siku ya Ijumaa,
msemaji wa upande wa kisiasa wa M23 Amani Kabasha aliituhumu serikali mjini
Kinshasa, kwa kuyahujumu jumla mazungumzo ya amani mjini Kampala. Wengi wa
wajumbe wa kundi la M23 ni Watutsi kutoka kundi la awali la waasi amabo
waliingizw akatika jeshi la taifa mwaka 2009, na baadae kuasi mwaka 2012,
wakidai kuwa Kinshasa ilishindwa kusimamia sehemu yake ya makubaliano.
Waasi walichukuwa udhibiti wa mji wa
Goma, ambao ndiyo mji mkuu wa jimbo la Kivu ya Kaskazini kwa zaidi ya wiki moja
mwishoni mwa uliyopita, kabla ya kujiondoa kutokana na shinikizo la kimataifa.
Serikali ya Kongo kwa muda mrefu imeishtumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi, na
wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamesema kuwa kamandi ya kundi la M23, iliongozwa
na waziri wa ulinzi wa Rwanda.
Mwanaharakati wa haki za binaadamu
alisema kuwa katika eneo la Kabagana, karibu na mpaka wa Rwanda, aliwaona
wanajeshi wa Rwanda wakiingia kuwasaidia M23. Kigali imekanusha vikali tuhuma
kwamba ilikuwa inawapatia silaha na kuwafadhili waasi -- na hata kuwasaidia kwa
kutumia vikosi vyake yenyewe.
Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga/afpe
Mhariri: Sekione Kitojo
Mhariri: Sekione Kitojo
Chanzo: DWswahili
No comments:
Post a Comment