Umoja wa Afrika umeishutumu serikali
ya Sudan kuwa inauzuwia ujumbe wa AU kuzuru Abyei, eneo lenye mafuta ambalo
linaaniwa na Sudan na Sudan Kusini.
Taarifa ya AU inasema ziara hiyo
imeakhirishwa mara mbili katika juma, kwa sababu za usalama ambazo zinaonesha
siyo sababu nzito.
Umoja wa Afrika unajaribu kupatanisha
baina ya nchi hizo mbili kuhusu swala la Abyei, ambalo halikupatiwa ufumbuzi
tangu Sudan Kusini ilipojitenga kutoka Sudan mwaka wa 2011.
Chanzo: BBCSwahili
No comments:
Post a Comment