Waokozi nchini Niger wanasema kuwa
wamepata miili 87 ya watu waliofariki baada ya magari yao kuharibika walipokuwa
wanajaribu kuvuka jangwa la Sahara.
Mmoja wa waliokuwa wanaendesha
shughuli ya ukozi Almoustapha Alhacen, alisema kuwa miili yao ilikuwa katika
hali mbaya ya kuharibika na kuwa ilikuwa imeliwa sehemu moja na wanyama pori.
Miili hiyo inaaminika kuwa ya
wafanyakazi wahamiaji na familia zao. Wengi walikuwa wanawake na watoto.
Niger ni kivukio kikubwa cha
wahamiaji wanaokuwa safarini kufika Kusini mwa Jangwa la Sahara kuelekea Ulaya.
Lakini wengi wa wanaofanikiwa
kukamilisha safari hiyo huishia kufanya kazi katika mataifa ya Afrika
Kaskazini.
Kulingana na Bwana Alhacen, moja ya
magari ambayo wahamiaji hao walikuwa wanatumia kwa usafiri, liliharibika
walipotoka mji wa Arlit mwishoni mwa mwezi Septemba, au mwanzoni mwa Oktoba.
Maafisa wa usalama pia wamesema kuwa
gari la pili liliharibika lilipokuwa njiani kurejea Arlit ili kutengenezwa.
Inaonekana kuwa miongomi mwa wasafiri
hao takriban watu 10 walisafari kurejea Arlit na kutoa taarifa ya wenzao
kukwama jangwani.
Iliarifiwa kuwa miili mitano
ilipatikana.
Mnamo siku ya Jumatano, wafanyakazi
wa kujitolea pamoja na wanajeshi, walipokuwa wanawatafuta wahamiaji hao,
wakafanikiwa kupata maiti zaidi umbali wa kilomita 10 kutoka katika mpaka wa Algeria.
Kati ya maiti 48 waliopatikana,
kulikuwa na miiili ya watoto na vijana na Alhacen alisema kuwa walikuwa
wanaelekea nchini Algeria kutafuta vibarua vya mishahara midogo sana.
Akizungumza kutoka katika kiwanda cha
kuchimba madini ya Uranium, Kaskazini mwa Agadez, aliambia BBC kuwa hiyo ndiyo
iliuwa siku mbaya kwake baada maishani mwake baada ya kupata miili hiyo.
Chanzo: BBCSwahili
No comments:
Post a Comment