“Wengine wawili
walikamatwa na kifikia adadi ya watu 13 na kwamba uchunguzi utakapokamilika
watafikishwa mahakamani.”PHOTO|FILE
Na Haika
Kimaro, Mwananch
Mtwara. Watuhumiwa 11 wa ugaidi
waliokamatwa wakifanya mafunzo ya kijeshi yenye asili ya kigaidi msituni Wilaya
ya Nanyumbu, Mtwara wamefikishwa katika mahakama ya Mkoa Mtwara na kufunguliwa
upya mashtaka baada ya kesi yao ya awali kuondolewa katika mahakama ya Wilaya
ya Nanyumbu.
Akisoma mashtaka, Wakili wa Serikali
Mfawidhi Mtwara, Ladislaus Komanya alisema shauri hilo limesomwa upya baada ya
kuhamishiwa Mahakama ya Mkoa kutoka Mahakama ya Wilaya.
Komanya alisema washtakiwa wote
wanakabiliwa na makosa mawili.
Kwa mujibu wa wakili huyo, kosa la
kwanza ni kuwa, kati ya Septemba 21 na 26 mwaka huu wanadaiwa kufanya
mkusanyiko usiokuwa halali wenye lengo la uvunjifu wa amani.
Shtaka la pili ni kufanya uchochezi,
ambapo Septemba 26 mwaka huu Wilaya ya Nanyumbu kwenye msitu walikutwa na
machapisho ya kanda za cd zenye video za uchochezi hali iliyowapelekea watu
kujengea hofu.
Mahakama ilielezwa kuwa upelelezi wa
shauri hilo bado haujakamilika na kuomba kupangiwa tarehe nyingine ya
kusikilizwa.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Mtwara,
Dynes Lyimo alisema dhamana ipo wazi kwa kila mmoja kuwa na wadhamini wawili
wakazi Mtwara watakaosaini mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh5 milioni
mmoja kati yao awe ni mtumishi wa Serikali ama taasisi inayotambulika na awe na
barua ya utambulisho toka kwa mtendaji wa Serikali ya Mtaa anakoishi.
Hakimu wa mahakama hiyo aliahirisha
kesi hiyo na kusema kuwa itatajwa tena Novemba 11 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Mtwara, Stephen Zelothe alisema kuwa watuhumiwa wengine wawili walikamatwa
na kifikia adadi ya watu 13 na kwamba uchunguzi utakapokamilika watafikishwa
mahakamani.
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment