Simba
jana ilionja machungu ya kufungwa katika mechi za Ligi Kuu ya Tanzania Bara
baada ya kuchapwa mabao 2-1na Azam FC katika mechi iliyopigwa Uwanja wa Taifa.
Kwa
matokeo hayo Azam sasa inaongoza ligi hiyo kutokana na kujikusanyia pointi
23,huku ikiiacha Simba nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 20 wastani mzuri wa
mabao ya kufungwa na sawa na Mbeya City yenye pointi 20 lakini imezidiwa mabao.
Mpira
ulianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu ambapo Simba ilipata bao dakika ya
21 kupitia kwa Ramadhan Singano 'Messi' baada ya kupokea pasi ya Zahoro Pazi.
Azam
nayo ilisawazisha bao hilo dakika ya 40 lililofungwa na Kipre Tchetche baada ya
kuunganisha krosi ya Erasto Nyoni na kumuacha kipa wa Simba, Abel Dhaira
akichupa bila mafanikio.
Kipindi
cha pili kilianza kwa Azam ku fanya mashambulizi ambapo dakika ya 47 ,Kipre
Tchetche aliachia shuti kali lakini likatoka nje ya lango.
Dakika
ya 60 Simba ilikosa bao la wazi ambapo Mombeki,alifumua kombora kali akiwa nje
ya 18 lakini likatoka nje ya lango la Azam.
Azam
ilijibu shambulizi hilo dakika ya 63 John Bocco akiwa na kipa aliteleza na kipa
kuuwahi na kuudaka.
Kipre
Tchetche aliiandikia Azam bao la pili, baada ya kukokota mpira na kumfunga tela
beki wa Simba,Adam Miraji aliyeshindwa kumkaba na kumhadaa kipa Dhaira na
kupiga mpira uliokwenda moja kwa moja wavuni.
Katika
mechi nyingine za ligi hiyo, Omari Mngindo anaripoti kutoka Uwanja wa Mabatini,
Chalinze kwamba Ruvu Shooting na Kagera zimetoka sare ya bao 1-1.
Ligi
hiyo inatarajia kuendelea tena leo katika Uwanja huo ambapo, Yanga itachuana na
Mgambo Shooting Tanga.
Nayo
Coastal Union iliichapa Mtibwa Sugar mabao 3-0 katika mechi ya ligi hiyo
iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga
No comments:
Post a Comment