Benki Kuu ya Tanzania (BoT)
PICHA|MAKTABA
Na Tausi Ally, Mwananchi
Dar es Salaam. Kada wa CCM, Rajabu
Maranda, binamu yake Farijala Hussein na wafanyakazi watatu wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT), Novemba 18, mwaka huu wanatarajiwa kuanza kutoa utetezi wao
katika kesi inayowakabili.
Kesi hiyo inahusisha wizi wa Sh 207
milioni za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) iliyopo BoT.
Wakili wa Serikali, Awamu Mbangwa,
jana aliliambia jopo la mahakimu watatu kuwa kesi hiyo, ilifikishwa kwa ajili
ya washtakiwa kuanza kutoa ushahidi.
Jopo linalosikiliza kesi hiyo,
linaoongozwa na Jaji John Utamwa, akisaidiwa na Jaji Ignas Kitusi na Jaji Eva
Nkya.
Mawakili wa utetezi, Wabeya Kung’e na
Rose Rutha, nao walisema kuwa kesi ilikuja kwa ajili ya wateja wao kuanza
kujitetea lakini mshtakiwa Rajabu Maranda hayupo na wakili wake Majura Magafu
hivyo waliomba iahirishwe.
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo,
Jaji Utamwa alikubali na kuahirisha kesi hiyo hadi Novemba 18, mwaka huu.
Washtakiwa Rajabu, Farijala na
wafanyakazi wa BOT, Ester Komu, Bosco Kimera na Imani Mwakosya kwa pamoja
wanakabiliwa na mashtaka ya kuwasilisha nyaraka za uongo, kughushi na kuiba
jumla ya Sh 207 milioni kutoka kwenye Akaunti ya EPA. Nyaraka hizo za kughushi
ni pamoja na hati za makubaliano ya kuhamishiwa deni kutoka Kampuni ya General
Marketing ya India kwenda Kampuni ya Rashas (T) ambazo inadaiwa walizutumia na
kuiba Sh 207,284,391.44.
Maranda na Farijala tayari
wanatumikia vifungo vya nyakati mbalimbali jela, baada ya kupatikana na hatia
katika kesi tatu zinazohusu wizi wa fedha za EPA.
No comments:
Post a Comment