Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano, Bw. Job Ndugai, amesema baadhi ya wabunge hawataki kuheshimu kanuni
na miongozo inayotolewa na kiti cha spika hivyo kusababisha vurugu za mara kwa
mara ndani ya Ukumbi wa Bunge.
Alisema upo umuhimu wa wabunge
kuheshimu kanuni hizo ili kuepusha vurugu zinazojitokeza, kutoa ushirikiano kwa
kiti cha spika na kuzingatia miongozo inayotolewa.
Bw. Ndugai aliyasema hayo Mjini
Dodoma jana kwenye kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Kituo cha
Televisheni ya Taifa (TBC) na kukanusha madai ya baadhi ya wabunge kudai kiti
cha spika hakitendi haki bungeni.
Aliongeza kuwa, wakati mwingine
wabunge wakiomba mwongozo, wanataka majibu yatolewe papo hapo mbali ya kujua
kanuni zinasemaje kuhusu miongozo hivyo wakati mwingine husababisha vurugu
zisizo na tija.
"Niwaombe wabunge wote hasa
wapinzani, washirikiane na kiti cha spika ili Bunge letu liendeshwe kwa amani,
si dhamira ya spika au Bunge kumtoa nje mbunge yeyote, kama tutafuata kanuni
kama inavyotakiwa hakutakuwa na vurugu," alisema.
Alisema kiti cha spika huzingatia
zaidi usawa na kutoa fursa kwa wabunge kuchangia mijadala mbalimbali
kikizingatia suala zima la jinsia (wanawake kwa wanaume).
Aliongeza kuwa, hadi sasa hakuna
muswada au mapendekezo yaliyofikishwa bungeni kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete
lakini kama yatafika, wananchi watajulishwa kuhusu jambo hilo.
Aliwataka wabunge kuacha utoro
bungeni badala yake wahudhurie vikao vya Bunge kwani ni aibu kuona viti vingi
vikiwa tupu badala ya kujazwa na wabunge.
Akilizungumzia Bunge la 13 lililoanza
Mjini Dodoma jana, Bw. Ndugai alisema Serikali imepeleka vipaumbele vikuu
vitatu ambavyo ni miundombinu, kilimo, viwanda na biashara.
"Hii ina maana kuwa, bajeti
kubwa ya mwaka ujao itakwenda kwenye miundombinu ambayo ni uboreshwaji wa reli,
ujenzi wa madaraja, barabara, usafiri wa anga, bandari, vivuko na miundombinu
ya majitaka," alisema.
Bw. Ndugai alisema licha ya Serikali
kupeleka vipaumbele hivyo, wabunge wanaweza kuviondoa na kuweka vyakwao ambavyo
wataona ni muhimu kutokana na faida zakeNAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya

wataona ni muhimu kutokana na faida zake
Chanzo: Majira
No comments:
Post a Comment