Aliyekuwa Rais wa Liberia Charles
Taylor atatumikia kifungo chake cha miaka 50 jela nchini Uingereza baada ya
kupatikana na hatia ya uhalifu wa kivita.
Haya ameyasema waziri wa sheria
nchini Uingereza Jeremy Wright.
Sweden na Rwanda
pia zilikuwa zimeomba kumfunga jela Taylor
katika ardhi yao
baada ya rufaa yake kukataliwa na mahakama mwezi jana.
Taylor alihukumiwa kifungo cha miaka 50
jela na mahakama maalum ya Umoja wa Mataifa kuhusu Sierra Leone, mjini Hague.
Iliamua kuwa makosa dhidi yake
yalithibtishwa bila tashwishi.
Alihukumiwa jela mwaka 2012 kwa
kuwasidia waasi waliofanya maasi makubwa dhidi ya watu wa Sierra Leone
wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Taylor, mwenye umri wa miaka 65,
alipatikana na hatia ya kuwapa waasi wa Revolutionary United Front silaha na
wao wakimpa almasi kutoka Sierra
Leone.
No comments:
Post a Comment