Wanamageuzi maarufu katika chama
tawala cha Sudan wametangaza kuwa wanatoka chamani kuunda chama kipya, ishara
kuwa mzozo umezidi ndani ya serikali.
Wanaharakati hao wamelalamika juu ya
ukandamizaji wa maandamano ya hivi karibuni ya kupinga kupanda kwa bei ya
mafuta nchini humo.
Piya wamekishutumu chama cha Kiislamu
cha National Congress kwamba kinakwenda kinyume na misingi yake.
Kati ya waliotoka ndani ya chama ni
aliyekuwa mshauri wa Rais Omar al-Bashir.
Mwandishi wa BBC mjini Khartoum
anasema serikali ya Sudan inapata shida kumudu uchumi unaozidi kuzorota, hasa
kwa sababu ya kukosa pato kutokana na mafuta baada ya Sudan Kusini kujitenga
mwaka wa 2011.
Chanzo:
BBCSwahili
No comments:
Post a Comment