Muhubiri
Deya amekataa kurejea Kenya kwa hofu ya kutotendewa haki
Mhubiri mkenya aliyedai kuwa na uwezo
wa kuwatunga mimba wanawake, kimiujiza, kupitia kwa maombi, ameshitakiwa kwa
makosa ya ubakaji nchini Uingereza.
Polisi walisema kuwa Gilbert Deya,
mwenye umri wa miaka 61, alishitakiwa wiki jana kwa kosa la ubakaji , kosa
lengine la jaribio la kumbaka mwanamke pamoja na kumnyanyasa kimapenzi msichana
mwenye umri wa miaka 14
Deya apokuwa Kenya alidai kuwa
anaweza kuwasaidia wanawake wenye matatizo ya kupata watoto kuweza kushika
mimba baada ya kuwaombea.
Kwa mujibu wa jarida la The Guardian
nchini Uingereza Mhubiri huyo alishitakiwa siku ya Ijumaa kwa makosa matatu na
kuzuiliwa kwa muda katika mahakama moja mjini London akisubiri kusikilizwa kwa
kesi yake tarehe nane mwezi Novemba.
Deya alitoroka nchini Kenya alipokuwa
anasakwa kwa madai wa kuwaiba watoto huku akiwahadaa wanawake kuwa angeweza
kuwatunga mimba kwa kuwaombea.
Mkewe ambaye walikuwa wanashirikiana
naye kwa kashfa hiyo alipatikana na na hatia ya wizi wa watoto na kwa sasa
anatumikia kifungo chake nchini Kenya.
Hata hivyo mnamo mwaka 2011 waziri wa
mambo ya ndani UingerezaTheresa May aliamuru mhubiri huyo kurejeshwa Kenya
baada ya mahakama kukataa ombi lake la rufaa kukataliwa akitaka asirejee Kenya.
Serikali ya Kenya inadai kuwa
aliwaiba watoto watano kati ya mwaka 1999 na mwaka 2004.
Wasiwasi ulizuka 2004 mara tu baada
ya kipindi kimoja cha BBC radio 4 cha udadisi kwa Jina Face the Facts
kupeperusha hewani shughuli zilizofanywa na Deya.
Wanawake ambao hawangeweza kutunga
mimba ama waliokuwa wamepita umri wa kuzaa, waumini katika kanisa lake la
Peckham Kusini mwa London waliahidiwa wataweza kupata watoto kimiujiza.
Lakini watoto hao walikuwa wanazaliwa
katika zahanati bandia mjini Nairobi nchini Kenya.
Chanzo: BBCSwahili
No comments:
Post a Comment