Liz
alibakwa na watu waliomtupa kwenye shimo la choo na kumvunja uti wa mgongo
Mamia ya waandamanaji nchini Kenya
wamewasilisha polisi hati ya kutaka kukamatwa kwa watuhumiwa waliombaka
msichana huyo wa miaka 16.
Msichana huyo alibakwa na kundi la
wanaume na kutupwa katika shimo la choo ambapo alivunjika mgongo wake.
Wanaume wanaotuhumiwa kumbaka
msichana huyo waliamriwa na polisi kukata nyasi kama adhabu ya kitendo hicho.
Hati hiyo ya kutaka kuwafungulia
mashitaka watuhumiwa wa ubakaji imetiwa saini na watu milioni 1.2 wakitaka
watuhumiwa kukamatwa haraka na kuwafikisha mahakamani.
Waandamanaji hao wameelezea
kukasirishwa na adhabu hiyo na kuhoji kwa nini polisi hawakufanya uchunguzi ili
kumtendea haki msichana huyo.
Pia wanataka polisi waliowaadhibu
washukiwa na kisha kuwaachilia, wakamatwe na kufunguliwa mashitaka.
Tayari wanawake milioni 1.2 wameunga
mkono kampeini hiyo iliyoanzishwa na mwanaharakati Nebila katika mtandao wa kijamii
wa Avaaz ulio na wanachama milioni ishirini na saba kote duniani na inaarifiwa
idadi ya wanawake wanaopinga kitendo cha wabakaji na kile cha polisi kuwaadhibu
kwa kukata nyasi, inaendelea kuongezeka.
Kampeini hii imekuja baada ya
msichana Liz kubakwa na genge la wanaume sita ambao baadaye walimtupa ndani ya
shimo la choo.
Liz alipata majeraha mabaya sana na
hata kuvunjika uti wa mongo na sasa amelazimika kutumia kiti cha magurudumu na
hadi sasa amefanyiwa upasuaji katika sehemu zake za siri.
Polisi waliwakamata watuhumiwa watatu
kati ya sita waliodaiwa kumbaka msichana huyo, lakini baadaye wakawaachilia
baada ya kuwaadhibu kwa kukata nyasi nje ya kituo cha polisi.
Chanzo: BBCSwahili
No comments:
Post a Comment