Melfu ya wakimbizi nchini Jamuhuri ya
Kidemokrasi ya Congo, wameingia nchini Uganda, huku majeshi ya serikali ya DRC
yakipambana vikali na waasi wa M23.
Makabiliano makali kati ya pande hizo
mbili yamepamba moto huku kukiripotiwa kutokea mashambulizi ya maombora karibu
na mji wa Bunagana ulio kati ya mpaka wa DRC na Uganda.
Msemaji wa shirika la kuwahudumia
wakimbizi la UNHCR, alisema kuwa wakimbizi elfu mbili wamevuka na kuingia
Uganda hii leo na kuifikisha idadi ya wakimbizi hao hadi elfu tano.
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa
mapema wiki hii alisema kuwa kundi la waasi la M23 lsio tisho tena la kijeshi
kufuatia ushindi kadhaa wa jeshi dhidi ya waasi hao ambapo waliweza kuthibiti
miji iliyokuwa imetekwa na waasi hao.
Aliongeza kuwa waasi hao wametoeroka
maeneo ya Bunagana na kwamba sasa wako katika kipnade kidogo cha ardhi karibu
na mpaka wa Rwanda.
Wanajeshi wa DRC wakisaidiwa na jeshi
la Umoja wa Mataifa( MONUSCO) walifanikiwa kudhibiti kambi ya kijeshi ya
Rumangabo siku ya Jumatatu
Chanzo: BBCSwahili
No comments:
Post a Comment