Polisi nchini Somalia wamevamia makao
makuu ya shirika la redio la Shebeelle, mjini Mogadishu, na hivo kukata
matangazo yake.
Polisi walidai kuwa kituo hicho cha
redio kilikuwa kinatumia jengo la serikali kinyume na sheria.
Askari waliokuwa na silaha
walizingira kituo hicho kilioko karibu na uwanja wa ndege wa Mogadishu, na
kuwakamata waandishi wa habari.
Siku nne zilizopita wizara ya mambo
ya ndani ya nchi iliitaka redio Shebelle ilihame jengo.
Wakuu walisema wanalichukua tena
jengo hilo ambalo ni la serikali.
Waandishi wa habari wa redio Shebelle
walikuwa wakitangaza habari kuhusu operesheni hiyo wakati jengo linavamiwa,
kabla ya jengo kufungwa kabisa.
Waandishi wa habari 6 wameuwawa
nchini Somalia mwaka huu
Chanzo: BBCSwahili
No comments:
Post a Comment