Mapambano
karibu na mji mkuu, Damascus
Wanajeshi wa serikali ya Syria leo
wamewavamia waasi karibu na mji mkuu, Damascus, na kuwaua wapiganaji wapatao 40
wa upinzani. Mji wa kaskazini wa Safira, kusini mashariki mwa Aleppo, pia
umeshambuliwa.
Kwa
mujibu wa ripoti za vyombo vya habari uvamizi huo ulikuwa sehemu ya operesheni
ya jeshi dhidi ya ngome za waasi zinazouzunguka mji huo, makao makuu ya utawala
wa rais wa nchi hiyo, Bashar al Assad. Uvamizi huo karibu na Damascus umefanywa
saa chache baada ya vikosi vya rais Assad kuuteka mji wa Hatitat al-Turkomen,
kusini mwa mji huo, na hivyo kudhibiti barabara muhimu inayouunganisha mji huo
mkuu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Damascus.
Shirika
la habari la serikali, SANA, limesema waasi 40 wameuwawa katika hujuma hiyo
iliyotokea karibu na eneo la Otaiba, na kwamba shehena kubwa ya silaha
imepatikana, yakiwemo makombora ya kuripua vifaru. Eneo hilo ni sehemu ya
ukanda unaojulikana kama Ghouta Masharki, ambako kulifanyika shambulizi la
silaha za sumu mwezi Agosti mwaka huu, ambapo mamia ya watu waliuwawa, wakiwemo
wanawake na watoto.
ATTENTION
EDITORS - VISUALS COVERAGE OF SCENES OF DEATH AND INJURY Syrian activists
inspect the bodies of people they say were killed by nerve gas in the Ghouta
region, in the Duma neighbourhood of Damascus August 21, 2013. Syrian activists
said at least 213 people, including women and children, were killed on
Wednesday in a nerve gas attack by President Bashar al-Assad's forces on
rebel-held districts of the Ghouta region east of Damascus. REUTERS/Bassam
Khabieh (SYRIA - Tags: CONFLICT POLITICS CIVIL UNREST) TEMPLATE OUT Maiti za
watu waliouwawa Ghouta na silaha za sumu
Afisa
mmoja wa jeshi ambaye jina lake halikutajwa, ameiambia televisheni ya taifa ya
Al-Ikhbariya kwamba wapiganaji wa kigeni ni miongoni mwa waliouwawa na
shambulizi hilo limefanywa baada ya kupata taarifa za kijasusi. "Ilikuwa
operesheni iliyofanikiwa. Tutaendelea kupata ushindi kutoka sehemu moja hadi
nyengine," akaongeza kusema afisa huyo.
Mwanajeshi
mwingine, ambaye hakutambulishwa kwa majina, amesema waasi ni wa kundi la Islam
Brigade na Jabhat al Nusra au Al Nusra Front, lenye mafungamano na mtandao wa
kigaidi wa al Qaeda. Shirika la haki za binaadamu la Syria lenye makao yake
jijini London, Uingereza limesema wapiganaji wapatao 20 wameuwawa katika
uvamizi huo, lakini halikutoa maelezo zaidi.
Wakati
huo huo, helikopta za jeshi zimeushambulia mji wa kaskazini wa Safira, kusini
mashariki mwa Aleppo. Kambi kubwa ya jeshi karibu na mji huo inaaminiwa ina
kituo cha chini ya ardhi cha kinachotumiwa kutengeneza na kuhifadhi silaha za
sumu. Shirika la madaktari wasio na mipaka limesema watu 130,000 wameukimbia
mji wa Safria mwezi huu na kwamba mji huo umekuwa ukishambuliwa kwa mabomu
tangu Oktoba 8. Taarifa ya shirika hilo imesema watu 76 wamekufa mjini humo.
Shambulizi
la bomu
Katika
tukio lengine la machafuko, shirika hilo limeripoti kuwa bomu lililokuwa
limetegwa ndani ya motokaa limelipuka nje ya msikiti katika kijiji cha Suq Wadi
Barada, na watu 40 ama wameuwawa au kujeruhiwa katika mlipuko huo. Hakuna
taarifa za idadi kamili ya watu waliouwawa au kujeruhiwa katika mji huo,
unaopatikana kaskazini magharibi mwa mji mkuu, Damascus.
Mkurugenzi
wa shirika la haki za binaadamu la Syria, Rami Abdel Rahman, amesema miongoni
mwa waliojeruhiwa ni watoto. Rahman aidha amesema ingawa mji huo uko mikononi
mwa waasi, wanajeshi wanaomtii rais Assad wameuzingira. Televisheni ya taifa
imeripoti juu ya shambulizi hilo, ikiwashutumu magaidi wenye mafungamano na al
Qaeda. "Waasi wa kundi la Al Nusra Front wamelipua bomu karibu na msikiti
wa Osama Bin Zeid katika kijiji cha Suq Wadi Barada katika mkoa wa Damascus.
Taarifa za awali zinasema watu wameuwawa na wengine kujeruhiwa,"
ikatangaza televisheni hiyo.
Mapambano
ya Wakurdi
Kuhusu
mapambano kati ya Wakurdi na wapiganaji wa jihad shirika hilo limesema
wapiganaji wa kikurdi wamezidi kusonga mbele katika mkoa wa Hassaekh wenye
idadi kubwa ya Wakurdi. Wapiganaji hao waliingia mji wa Yaaroubiyeh leo na
kukabiliana na makundi kadhaa ya jihad, yakiwemo Islamic State of Iraq na Al
Nusra Front, yenye mafungamano na kundi la al Qaeda.
A
Kurdish female fighter from the Popular Protection Units (YPG) carries a walkie-talkie
as she stands near fellow fighters carrying their weapons and using binoculars
in the Kurdish town of Ifrin, in Aleppo's countryside October 14, 2013. Kurds
comprise around 10 percent of Syria's 23 million population. They are
concentrated in Ifrin and other areas of the northwest, in parts of Damascus
and in the northeastern oil producing area of Qamishli, where there has also
been intense fighting between Kurds and al-Qaeda linked Islamic State of Iraq
and the Levant fighters. Picture taken October 14, 2013. REUTERS/Roshak Ahmad
(SYRIA - Tags: POLITICS CIVIL UNREST CONFLICT) Wapiganaji wa Kikurdi nchini
Syria
Mji
wa Yaaroubiyeh unaodhibitiwa na waasi uko katika kivuko kikuu cha mapakani
kuingia nchini Iraq na kuuteka mji huo kutawapa wapiganaji wa Kikurdi njia
rahisi ya kusafirishia bidhaa na mahitaji mengine kutoka eneo la Wakurid
kaskazini mwa Iraq. Eneo hilo limeshuhudia mapiganao makali katika siku za
nyuma na mapambano makali kati ya wapigaji wa Kikurdi na wapiganaji wa makundi
ya jihad kaskazini mwa Syria yamesababisha vifo vya mamia ya watu katika miezi
iliyopita.
Pia
mwezi Machi mwaka huu wanaume waliokuwa wamejihami na bunduki waliwaua
wanajeshi 51 wa Syria baada ya kuvuka na kuingia Iray kutoka Yaaroubiyeh.
Wanajeshi hao walikuwa wameingia Iraq kutafuta hifadhi kufuatia mapambano na
waasi upande wa Syria wa mpaka.
Mwandishi.
Josephat Charo/APE/AFPE
Mhariri:
Daniel Gakuba
Chanzo:
DWSwahili
No comments:
Post a Comment