Wafuasi
wa Muslim Brotherhood wakiandamana kupinga kuondolewa kwa Rais Mohammad Morsi
Vyombo vya habari vya Misri
vinaripoti kuwa serikali ya nchi hiyo imemtia mbaroni mwanasiasa maarufu Essam
El Arian ambaye pia alikuwa ni mwanachama wa Muslim Brotherhood na Makamu
Mwenyekiti wa chama cha Justice and Freedom ambacho pia ni sehemu ya
Muslim Brotherhood.
Bwana El Arian ametiwa mbaroni katika
mji mkuu wa Kairo.
Hapo awali mwendesha mashtaka wa nchi
hiyo aliagiza Essam El Arian akamatwe tangu mwezi July baada ya Rais Mohammad
Morsi ambaye pia alikuwa ni mwanachama wa Justice and Freedom
kuondolewa madarakani.
Kukamatwa kwa kiongozi huyo ni moja
ya hatua ya serikali iliyopo madarakani kudhibiti hatakati zinazoendeshwa na
kundi hilo lenye itikadi kali za kiislamu ambazo zimepigwa marufuku.
Shirika la habari la serikali la
Misri, Mena, limesema Bwana Erian anatarajiwa kufikishwa mahakamani wiki ijayo
pamoja na Rais aliyoondolewa madarakani Mohammad Morsi na maafisa wengine wa
Muslim Brotherhood.
Msemaji wa Muslim Brotherhood
ameimbia BBC kuwa Bwana Erian alikamatwa siku ya jumatano akiwa nyumbani kwake
mjini Cairo.
Picha zilizosambazwa kwenye vyombo
vya habari vya Misri zinaonyesha kitendo cha kukamatwa kwake ambapo Bwana Erian
anaonekana akiwa na tabasamu amesimama karibu ni mifuko miwili.
Mwandishi wa habari wa BBC aliyepo
Cairo Orla Guerin anasema kabla ya Bwana Erian kwenda mafichoni alikuwa ni
mwanachama maarufu wa Muslim Brotherhood.
Chanzo: BBCSwahili
No comments:
Post a Comment