WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli
amesema tatizo la uzidishaji wa mizigo unaofanywa na magari makubwa iwapo
litaendelea, barabara zote zitaharibika. Dk. Magufuli alitoa kauli hiyo bungeni
jana, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed
(CUF).
Katika swali lake, Hamad alitaka
kujua sababu ya barabara zinazojengwa kuharibika ndani ya kipindi kifupi.
Dk. Magufuli alisema tatizo la
kuharibika kwa barabara linasababishwa na ujenzi duni wa wakandarasi, lakini
kwa kiasi kikubwa huharibiwa na magari yanayozidisha mizigo.
"Kwa mfano katika Barabara ya
Dar es Salaam hadi Dodoma tayari upande wa kushoto wa barabara umeshabonyea.
"Kwa Tanzania uzito unaotakiwa
kupita barabarani hautakiwi kuzidi tani 56, lakini magari yanazidisha hadi kati
ya tani 90 na 98, tukiendelea hivyo si tu barabara zitavimba bali zitapasuka
kabisa," alisema.
Alitoa viwango vya uzito unaotakiwa
katika nchi kama Marekani kuwa ni tani 36.2, Uingereza Tani 44, Ufaransa Tani
40 na Ujerumani ni Tani 40.
Awali akijibu swali la msingi la
Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige, Dk. Magufuli alisema Mkoa wa Geita umeingia
mkataba na Mhandisi Mshauri kwa ajili ya kuifanyia marekebisho barabara ya
Geita, Bukoli hadi Kahama.
Alisema mkataba huo ni kwa ajili ya
kuifanyia upembuzi yakinifu pamoja na usanifu wa kina barabara hiyo kwa gharama
ya Sh milioni 403.9 katika kipindi cha miezi 13.
Katika swali lake, Maige alitaka
kujua lini utekelezaji wa kuiwekea lami barabara hiyo utaanza. Chanzo:
mtanzania
No comments:
Post a Comment