Kansela Angela Merkel na rais
Francois Hollande.
Baada ya madai ya kudukukuliwa kwa
simu ya mkononi ya Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na idara ya usalama wa
Taifa ya Marekani NSA, washiriki wa mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya
wanataka hatua zichukuliwe.
Ingawa suala la ulinzi wa data na
uendelezaji wa uchumi wa digitali lilikuwa miongoni mwa ajenda za mkutano mkuu
wa viongozi wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels Ubelgji, hakuna aliejua kuwa
lingepata umuhimu wa kipekee kabla ya mkutano huo.
Lakini sakata la udukuzi wa
mawasiliano ya simu ya mkononi ya Kansela Angela Merkel limebadili mambo, na
washiriki wa mkutano wanataka hatua zichukuliwe. Hadi jioni ya Jumatano,
Ufaransa na Ujerumani zilikuwa na mitizamo tofauti juu ya taarifa kuwa idara ya
Usalama wa taifa ya Marekani NSA ilikuwa imeyadukuwa mawasialiano ya raia wa
Ulaya.
Barroso ailinganisha NSA na Stasi
Baada ya udukuzi huo kumgusa Kansela Merkel mwenyewe, kila kitu kilibadilika ghafla, na sasa Berlin na Paris zimeungana pamoja katika kuelezea kughadhabishwa na udukuzi huo. Rais wa halmashauri ya Ulaya Jose Manuel Barosso, alikwenda mbali na kuyiita tabia ya Marekani kuwa ni ya kiimla.
Baada ya udukuzi huo kumgusa Kansela Merkel mwenyewe, kila kitu kilibadilika ghafla, na sasa Berlin na Paris zimeungana pamoja katika kuelezea kughadhabishwa na udukuzi huo. Rais wa halmashauri ya Ulaya Jose Manuel Barosso, alikwenda mbali na kuyiita tabia ya Marekani kuwa ni ya kiimla.
Rais wa Halmashauri ya Ulaya Jose
Manuel Barroso.
"Tunafahamu hapa Ulaya nini
maana ya utawala wa kiimla, na tunajua kinaochotokea pale serikali inapotumia
madaraka yake kuingilia maisha ya watu. Kwa hivyo hili ni suala muhimu sana
siyo kwa Ujerumani tu bali kwa Ulaya nzima - haki ya faragha, na ulinzi wa
taarifa," alisema Barroso akiilinganisha NSA na shirika la ujasusi la
iliyokuwa Ujerumani Magharibi.
Pia katika bunge la Ulaya, Kansela
Merkel amepata uungwaji mkono na pia shinikizo, kutafakari juu ya athari za
udukuzi wa mawasiliano si kwake tu bali pia kwa raia wote. Mbunge wa chama cha
Kiliberali FDP Nadia Hirsh amemtaka Kansela Merkel kuonyesha sasa kuwa
anawajali raia wake na siyo hadi yeye ageuke mwathirika ndiyo aonyeshe kujali.
Schulz: Mazungumzo ya biashara huru
yasitishwe
Martin Schulz, ambaye ni rais wa
Bunge la Ulaya na anaepewa nafasi ya kumrithi Barroso kama rais wa Halmashauri
ya Ulaya, yeye ametaka hata mazungumzo juu ya makubaliano ya biashara huru kati
ya Marekani na mataifa ya Ulaya yasitishwe kwanza.
"Mimi naamini sasa laazima
kuwepo na wakati wa kusimama na kutafakari. Ninapokwenda kwenye mazungumzo na
naanza kuhofia kuwa wenzangu katika upande wa pili, tayari wanajua kupitia
ujasusi, kile ninachotaka kusema katika majadiliano, hapo kunakuwa hakuna usawa
tena.
Rais wa Bunge la Ulaya Martin Schulz
. Rais wa Bunge la Ulaya Martin Schulz .
Kwa hivyo naamini laazima kwanza
tuzungumze na marafiki zetu Wamarekani juu ya viwango tunavyopaswa
kulinda," alisema mwanasiasa huyo wa chama Social Democratic SPD cha hapa
Ujerumani.
Siku ya Jumatano, saa chache kabla ya
taarifa za udukuzi julikana, bunge la Ulaya, lilikuwa limepiga kura kusitisha
mkataba wa mfumo unaojulikana kama SWIFT, ambao kupitia kwake, taarifa za
kibenki za raia wa Ulaya hukabidhiwa kwa Marekani.
Lengo la mfumo huu ni kupambana na
ugaidi, lakini wabunge wengi waliona kuwa unakiuka haki za faragha. Kabla ya
sakata ka udukuzi kura dhidi ya mfumo wa SWIFT haikuwa na madhara makubwa kwa
sababu serikali nyingi ambazi zinafaa kuridhia hatua hiyo, zinathamini zaidi
suala la usalma kuliko udukuzi, lakini sasa upepo umebadilika kwa kiasi
kikubwa.
Mada nyingine zafunikwa
Kabla ya matukio ya hivi karibuni,
wengi walitarajia mkutano wa kawaida. Wakati wa mkutano huo, viongozi
walitarajia kupiga hatua katika majadiliano ya kuedeleza muungano wa kichumi na
kifedha inagawa hawakutemegea kufanya maamuzi yoyote ya msingi.
Viongozi wa Umoja wa Ulaya wakiteta
jambo wakati wa mkutano wa kilele wa Umoja huo. Viongozi wa Umoja wa Ulaya
wakiteta jambo wakati wa mkutano wa kilele wa Umoja huo.
Hata hivyo, suala la wakimbizi,
ambalo Italia ililiweka katika ajenda ni la muhimu zaidi kuliko udukuzi, kwa
sababu ni jambo la kufa na kupona kwa wahamiaji. Licha ya hivyo, hakutarajiwi
kuwepo na mabadiliko makubwa katika sera ya wakimbizi ya Umoja wa Ulaya, kwa
kuwa mataifa ya kaskazini hayataki kujihusisha na wakimbizi kabisaa.
Lakini kwa kulinganisha na maafa
katika bahari ya Mediterranean, wakosoaji wanauona udukuzi wa Marekani kuwa ni
jambo hafifu, hata kama simu ya Kansela wa Ujerumani ilidukuliwa.
Mwandishi: Christoph Hasselbach/DW
Brüssel
Tafsiri: Iddi Ismail Ssessanga
Mhariri: Daniel Gakuba
Chanzo: DWSwahili
No comments:
Post a Comment