Mabaki ya basi la abiria lililogongwa
na treni jijini Nairobi
Kiasi ya watu 12 wameuawa baada ya treni la abiria kuligonga
basi lililokuwa likivuka reli jijini Nairobi, Kenya. Shirika la Msalaba
Mwekundu la Kenya limesema watu wengine wamejeruhiwa kufuatia ajali hiyo mbaya
Ajali za barabarani zinazosababisha
idadi kubwa ya vifo hutokea kila mara nchini Kenya. Kuna ukiukwaji mkubwa wa
sheria za barabara na mabasi yanayojaa abiria kupinduka, kila mara huendeshwa
kwa mwendo wa kasi na kuyapita magari mengine ili kupata faida ya haraka.
Kwa mujibu wa walioshuhudia, gari
hilo lilikokotwa kwa takribani mita 500 kutoka eneo la ajali. Mkuu wa polisi
jijini Nairobi Benson Kibui amesema basi hilo la abiria lilivuka reli wakati
treni hilo lilipofika kwa mwendo wa kasi. Ajali hiyo ilitokea wakati wakaazi
wengi wa jiji walipokuwa wamejaa barabarani wakielekea makazini saa za asubuhi.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri:Josephat Charo
No comments:
Post a Comment