Waziri
Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye, ameunga mkono kauli ya
Rais Jakaya Kikwete, kuhusu kukithiri kwa rushwa ndani Chama Cha Mapinduzi
(CCM) na kuwa ndiyo moja ya sababu ya wananchi kukasirika na kukichukia chama.
Akizungumza
na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Sumaye, alisema yeye alianza muda mrefu
kuzungumzia rushwa, hivyo anashukuru Rais kuzungumzia vitendo hivyo.
"Namuunga
mkono Rais, tupambane na rushwa kwenye uchaguzi na mahali popote pale... Rais
amefanya vizuri sana," alisema Sumaye na kuongeza;
"Wapo
wanaosema Rais anazungumza tu, kiongozi lazima azungumze kwanza na baadaye
matendo yafuate... waliopo chini yake wataanza kuchukua hatua (kuwajibika) na
watakaobaki yeye (Rais) atawachukulia hatua wenye matatizo."
Alisema
mkuu wa nchi na Chama akizungumzia jambo baya ni lazima aungwe mkono.
"Haiwezekani ni mshangae , namuunga mkono kwani ni dhahiri kabisa
tusipomuunga mkono wananchi watatukataa," alisisitiza Sumaye.
Alipoulizwa
kama kuna uwezekano wa CCM kupoteza majimbo mengi katika uchaguzi ujao, Sumaye
alisema hilo lipo dhahiri.
"Wananchi
wengi hawapendi rushwa hata kidogo, kwani hawanufaiki nayo, tukiendekeza rushwa
wananchi watakiadhibu chama chetu." alifafanua. Alisema yeye anapiga
rushwa ndani ya CCM, ndani ya chama chochote kile ndani ya Serikali.
Alipoulizwa
sababu za vyama vya upinzani kuzidi kukua kwa kasi, Sumaye alisema;
"Tukiweka viongozi ambao hawamudu nafasi na hasa kama wamezipata kwa
rushwa watu wanakasirika, wakikuchukia wanakunyima kura."
Alitaja
sababu nyingine kuwa ni viongozi wa CCM wa mikoa na kwingineko hawaendi kwa
wananchi matokeo yake wanapoteza
mvuto
wa chama. Alitaja sababu nyingine kuwa watu wamezidi kuelimika tofauti na
ilivyokuwa zamani.
"Zamani
mpinzani alionekana kama mhalifu, lakini sasa anaonekana kama yupo ndani ya
chama tawala, jambo ambalo ni zuri," alisema.
Alisema
kama alivyobainisha Rais Kikwete, hivi sasa vinara wa rushwa ndio wanaonekana
watu wa maana na kupokewa kwa nderemo kila wanapopita ndani ya jamii.
Alisema
kama wana CCM watapuuza kauli hiyo ya Rais Kikwete na kuwaruhusu watoa rushwa
kushika dola, chama hicho kitakuwa kimejichimbia kaburi refu lililomiminwa
zege.
Sumaye
alisema kauli ya Rais Kikwete ina mantiki kubwa kwa chama hicho na taifa kwa
ujumla na kama itafanyiwa mzaha CCM itaangamia.
Sumaye
alisema hivi karibuni amepanga kuitisha mkutano wa vyombo vya habari jijini Dar
es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine, atatoa tamko rasmi la kuunga mkono
kauli ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete kupambana na vitendo viovu vya rushwa
vinavyofanywa na baadhi ya watu wenye malengo ya kugombea urais, ubunge na
udiwani katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015.
Hivi
karibuni Rais Kikwete, alielezea kusikitishwa na kukithiri kwa vitendo vya
rushwa ndani ya chama hicho na kuonya kuwa hali hiyo ikiendelea itaathiri Cham
No comments:
Post a Comment