Wakuu wa idara ya Polisi nchini Kenya
wamewaonya waandisi wa habari kuhusu walivyoripoti matukio katika jumba la
Westgate ambako magaidi walishambulia zaidi ya wiki tatu zilizopita.
Onyo hili linakuja baada ya taarifa
za wanajeshi kufanya uporaji katika jengo hilo wakati wakipambana na magaidi
hao waliokuwa wamewateka nyara watu waliokuweme ndani ya jumba hilo.
Mkuu wa polisi, David Kimaiyo alisema
kuwa waandishi hawapaswi kutoa kuchochea Propaganda, au kuwachochea wakenya
wakati wakipeperusha matangazo yao.
Duru zinasema kuwa baadhi ya
waandishi wa habari wamehojiwa na polisi hii leo.
Picha za CCTV zilizofichuliwa kwa
waandishi wa habari zilionyesha wanajeshi wakitoka ndani ya jumba hilo na
mifuko ya plastiki zilizoshukiwa kuwa na bidhaa kutoka katika mojawapo ya
maduka makubwa yaliyokuwa ndani ya jengo hilo la Nakumatt.
Hata hivyo jeshi limekanusha madai
hayo na kusema kuwa wanajeshi walikuwa wanachukua maji ya kunywa wakati wa
operesheni yao dhidi ya magaidi.
Takriban watu 67 walifariki ikiwemo
wanajeshi na mamia ya wengine kujeruhiwa kwenye shambulizi hilo liliosababishwa
na Al Shabaab kama walivyokiri. Waliwateka nyara watu ndani ya jingo hilo kwa
siku nne.
Pamoja na kupora, vyomo vya habari
Kenya vimesema kuwa baadhi ya wanajeshi waliuwana na wenzao wakati wa
operesheni yao kutoka na kile kilichosemekana kuwa ukosefu wa maelekezo mazuri
kuoka kwa wakuu wa usalama.
Chanzo: BBCswahili
No comments:
Post a Comment