MWENYEKITI wa Chama cha Waandishi wa
Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Abbas Pinto ametoa taarifa kwa vyombo
vya Habarii juu ya sababu za kuwania kwake Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), hii hapa;
"Ndugu waandishi nagombea nafasi
ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji katikauchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) kupitia Kanda ya Pwani na Morogoro na nimeamua kugombea nafasi
hiyo ili kuleta mabadiliko ya kweli na kuleta fikra endelevu.
Naamini kabisa nikichaguliwa katika
nafasi hiyo kwa kushirikiana na viongozi wenzangu tutaleta mafanikio zaidi na
hususani kupokea kijiti kwa viongozi wenzetu waliotangulia ambao wameweka mfumo
mzuri wa utawala bora ndani ya shirikisho.
Ili mafanikio yaweze kupatikane ni
lazima tuweke mpango endelevu kwa kuwekeza zaidi katika soka la vijana, kuandaa
kozi ,warsha na makongamano yatakayotupa dira nzuri ya kukuza na kuwaendeleza
vijana na mchezo wenyewe wa soka.
Kikubwa ambacho nitahakikisha
ntalisimia kidedea ni kuendeleza vipaji vya wachezaji chipukizi, kuandaa
makocha, waamuzi chipukizi na upatikanaji wa vifaa vya michezo ikiwemo
kuhakikisha viwanja vya michezo havitumiki kwa matumizi mengine na hivi
vilivyopo viweze kuboreshwa zaidi.
Lingine ni kuhakikisha mikoa yote
nchini inapata haki sawa katika kugawiwa rasilimali zinazopatikana kutoka kwa
wadhamini na Shirikisho la kandanda duniani (FIFA) na kuhakikisha mfumo wa
kutumia tiketi za elektroniki unaanza kutumika mara moja.
Mfumo huo utasaidia kumaliza tuhuma
za ubadhirifu wa mapato ya milangoni katika mechi mbalimbali zinazofanyika
nchini katika viwanja mbalimbali.Zinapopatikana pesa kwa wingi ndio
tutakapoweza kutumia fursa hiyo kufanya maendeleo ya mpira wa miguu.
Nafahamu majukumu mazito ambayo
yanatakiwa kutekelezwa na kamati ya utendaji na nikiwa kama mjumbe nafahamu
nchi yetu ambayo imekuwa ikikumbwa na changamoto mbalimbali katika uendelezaji
wa michezo hasa mchezo wa soka.
Kwa miaka 13 iliyokaa Uingereza
niliweza kupata nafasi ya kufanya kazi (Part time) pale BBC Swahili kwa kweli
niliweza kupata ufahamu wa hali ya juu sana kuhusu mpira wa miguu na kufanya
utafiti wa kina katika michezo ikiwa ni pamoja na wachezaji wake, viwanja,
kanuni na mbinu mbalimbali.
Lakini mwaka 1999 niliweza kupata
semina ya siku 45 nchini Brazili juu ya uongozi wa mpira wa miguu (Football
Administration), hatua ambayo ilinipata weledi mkubwa sana katika uongozi wa
mchezo wa mpira wa miguu.
Nina uhakika kwa hayo yote
niliyoyapata kabla na baada ya kuondoka nchini, yameweza kunipa mwanga sahihi
wapi tunapotakiwa kwenda, lakini pia kupata fursa ya kuweza kutumia uzoefu
wangu na hiki nilichokipata kuweza kutumia ndani ya TFF.
Hivyo nimeamua kuingia TFF ili
kutumia uzoefu wangu katika kuleta mabadiliko ya kweli, pamoja na kuwa mchezaji
wa timu ya Pan African mwaka 1993, pia na mchezaji wa timu ya Taifa ya Vijana
mwaka 1994.
Lakini kwa hivi sasa ni mjumbe wa
Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Chama Cha
soka mkoa wa Pwani, Mjumbe wa kamati ya masoko ya TFF na Mwenyekiti wa Chaa Cha
Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA)."
Chanzo: Dina Ismail
No comments:
Post a Comment