Mapigano yaongezeka Congo
Mapigano mapya yamezuka jana Jumamosi(26.10.2013) kati ya
majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na waasi katika siku ya pili ya
machafuko ambayo yamesababisha miito ya utulivu kutoka kwa jumuiya ya kimataifa
.
Mapigano
ya hivi karibuni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo yamezuka siku ya
Ijumaa, chini ya wiki moja baada ya serikali mjini Kinshasa na waasi wa kundi
la M23 kutangaza kuwa mazungumzo ya amani mjini Kampala yamevunjika.
Jeshi
la serikali jioni ya Jumamosi lilisema kuwa limeukamata mji wa Kibumba , mji
ulioko kilometa 25 kaskazini ya eneo mji wa mashariki mwa nchi hiyo wa Goma
ambao unatoa njia kuelekea katika eneo la waasi upande wa kaskazini.
Government
troops ride on a vehicle towards the frontline where they are fighting against
M23 rebels outside the eastern Congolese city of Goma, July 25, 2012.
Congolese
rebels and government forces traded heavy weapons fire around two eastern
villages on Friday, forcing thousands of civilians to flee towards the
provincial capital days ahead of a regional summit due to tackle the rebellion.
REUTERS/James Akena (DEMOCRATIC REPUBLIC OF CONGO - Tags: CIVIL UNREST POLITICS
CONFLICT) Wanajeshi wa serikali Congo
"Kibumba
uko chini ya udhibiti wa jeshi la serikali FARDC kuanzia leo," afisa
mwandamizi wa jeshi ameliambia shirika la habari la AFP mjini Goma. Waasi
hawakuweza kupatikana mara moja kuzungumzia tamko hilo.
Upande
mwingine wa mapigano umeanza ghasia siku ya Jumamosi wakati jeshi
liliposhambulia maeneo ya kundi la M23 katika jimbo la Mabenga, kiasi ya
kilometa 80 kaskazini mwa goma na karibu na mpaka na Uganda.
Jeshi
"limeanzisha mashambulizi katika barabara ya Mabenga kuelekea Kahunga.
Linatumia wanajeshi, vifaru na makombora", afisa mwingine wa jeshi
amesema, akizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina.
Waasi
wamethibitisha kuwa mapigano yamesambaa hadi katika eneo la kaskazini.
Mapigano
yasambaa
"Mapigano
yanaongezeka katika maeneo yote," kiongozi wa kisiasa wa M23 Bertrand
Bisimwa amesema katika tovuti ya kundi hilo.
Mjumbe
maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika mzozo huo, Mary
Robinson na Martin Kobler, wametoa taarifa wakielezea wasi wasi wao mkubwa
kuhusiana na mapigano hayo mapya.
UN
secretary general Ban Ki-Moon (L) signs a guestbook next to Congolese Senate
president Leon Kengo Wa Dondo (2nd L) in the Parliament in Kinshasa on May 22,
2013. Ban Ki-moon wraps up a visit to Mozambique and arrives in Kinshasa on a
key leg of his Africa trip centred on restoring peace in eastern Democratic
Republic of Congo where a flareup in fighting over the past days has left 19
dead. AFP PHOTO/JUNIOR D.KANNAH (Photo credit should read Junior D.
Kannah/AFP/Getty Images) Katibu mkuu wa UM Ban Ki Moon
"Tunatoa
wito kwa pande zote kuonyesha hali ya uvumilivu na kuanza tena majadiliano
mjini Kampala," wamesema. Marekani imesema kuwa imesitushwa na ripoti za
kuongezeka kwa mapigano, licha ya miito ya kimataifa kwa pande hizo kuonesha
hali ya kuvumiliana.
"Tunawasi
wasi mkubwa juu ya ripoti za mapigano ya mpakani, " katika jimbo la Kivu
ya kaskazini, msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni Jen Psaki amesema katika
taarifa, akizitaka pande zinazopigana, "kuacha vitendo vitakavyozidisha
hali hiyo".
Taarifa
ya Psaki imezitaka pande hizo kurejea katika majadiliano, " ili kuondoa
vikwazo vilivyobaki kuelekea kutiwa saini kwa makubaliano ya mwisho, na ya
msingi, ambayo yataleta usitishaji wa kudumu wa mapigano na kuwawajibisha wake
ambao wamefanya uhalifu mkubwa".
Jumuiya
ya kimataifa yaonya
Mkuu
wa sera za mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton pia ametoa wito,
"kwa wahusika wote katika eneo hilo kuzuwia kuongezeka zaidi kwa hali hiyo
na kuufanya mzozo huo wa kimataifa".
Athari
zilizoripotiwa ndani ya mpaka wa Rwanda kutokana na matukio ya hivi karibuni
yanapaswa kufanyiwa uchunguzi kwa pamoja," amesema Ashton.
European
Union High Representative for Foreign and Security Policy Catherine Ashton
speaks to journalists prior to a meeting of Ministers for Foreign Affairs in
the Palace of the Grand Dukes of Lithuania in Vilnius on September 6, 2013. AFP
PHOTO / TOMAS LUKSYS (Photo credit should read TOMAS LUKSYS/AFP/Getty Images)
Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya ,Catherine Ashton
Waasi
wanadai kuwa jeshi la serikali lilishambulia maeneo yao mapema siku ya Ijumaa,
lakini jeshi la serikali linasisitiza kuwa lilishambuliwa kwanza, madai ambayo
yanaungwa mkono na duru kutoka ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa
nchini humo, MONUSCO.
Wakati
huo huo jeshi la serikali ya Congo limesema limepata mafanikio makubwa dhidi ya
waasi wa M23 katika siku ya pili ya mapigano makali jana Jumamosi na kuitaka
nchi jirani ya Rwanda kusaidia kuwanyang'anya silaha waasi.
Mwandishi:
Sekione Kitojo / afpe
Mhariri:
Idd Ssessanga
No comments:
Post a Comment