Shughuli ya kuhesabu kura inaendela na huenda ikamalizika
baada ya wiki moja
Waangalizi wa kimataifa wameutaja
uchaguzi wa urais nchini Madagascar kuwa huru na wa haki huku matokeo ya
uchaguzi huo yakiendelea kusuburiwa.
Uchaguzi wenyewe uliofanyika siku ya
Ijumaa ulikuwa wa kwanza tangu mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika kisiwani humo
mwaka 2009.
Matokeo ya mwanzomwanzo yanaonyesha
mshirika wa rais aliyeng’olewa madarakani Marc Ravalomanana akiwa mbele kwa
hesabu za kura.
Richard Jean-Louis Robinson ana
asilimia 30 ya kura hadi sasa huku mshindani wake, Hery Martial Rakotoarimanana
Rajaonarimampianina akipata asilimia kidogo zaidi ya 15%.
Matokeo rasmi huenda yakajulikana
baada ya wiki moja.
Ikiwa hakuna mgombea yeyote atapata
zaidi ya asilimia 50, ya kura zilizopigwa, duru ya pili itafanyika tarahe 20
Disemba.
Mkuu wa uangalizi wa uchaguzi kutoka
Muungano wa Ulaya, Maria Muniz de Urquiza, amesema kuwa uchaguzi huo ulikuwa
huru na wa haki licha ya visa kadhaa vya ghasia.
Naye Nandi-Ndaitwah, mwangalizi mkuu
wa uchaguzi kutoka kanda ya Afrika Kusini, alisema uchaguzi huo ulikuwa huru na
wenye amani , wazi na kuwa unaonyesha matarajio ya watu.
Wagombea wakuu wawili, wameahidi
kuujenga upya uchumi wa Madagascar baada ya miaka mingi ya vurugu za kisiasa.
Zaidi ya 92% ya watu milioni 21
nchini humo wanaishi kwa dola mbili kwa siku , kulingana na benki ya dunia.
Bwana Rajaonarimampianina amesema
kuwa ana nia ya kuwasaidia vijana wasio na ajira , kujenga upya miundo msingi
na kuimarisha kilimo , kufanya mageuzi katika sekta ya elimu pamoja na
kuimarisha demokrasia nchini humo.
Bwana Robinson anasema kuwa mpango
wake wa maendeleo unatokana na ule wa Rais wa zamani Bwana kujaribu kujenga
upya sekta ya utalii inayokumbwa na changamoto si haba nchini humo.
Madagascar imekuwa ikikumbwa na
vurugu za isiasa tangu mwaka 2009, wakati Andry Rajoelina alipompindua kutoka
mamlakani, aliyekuwa Rais Marc Ravalomanana.
Mapinduyzi ya kijeshi yalisababisha
nci hiyo kutengwa na jamii ya kimataifa, na hata kunyimwa misaada.
Lakini mapema mwaka huu Bwana
Rajoelina na Ravalomanana walikubali kutoshiriki uchaguzi mkuu kulingana na
mpango ulioafikiwa na muungano wa SADC.
Chanzo: BBCSwahili
No comments:
Post a Comment