Polisi wa Misri wamefyatua moshi wa
kutoza machozi kuvunja maandamano mjini Cairo, ya wanafunzi wanaomuunga mkono
rais wa zamani, Mohamed Morsi.
Mawe yalirushwa na pande zote mbili
huku wanafunzi mia kadha wakijaribu kutoka chuoni kuelekea Medani ya Rabaa,
pahala pa kambi ya wafuasi wa Morsi ambayo ilifungwa na wakuu miezi miwili
iliyopita.
Hii ni siku ya pili ya mapambano
katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar, ambako kuna wafuasi wengi wa chama cha Muslim
Brotherhood cha Bwana Morsi.
Bwana Morsi aliondolewa madarakani na
jeshi mwezi wa Julai.
Chanzo: DWswahili
No comments:
Post a Comment