Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika
Jamhuri ya Demokrasi ya Congo unasema unasikitika kuwa watu waliofanya ukatili
katika mji wa Minova mwaka jana hawakufikishwa mahakamani.
Umoja wa Mataifa unasema una ushahidi
wa kesi 135 za ubakaji pamoja na mauaji na wizi wa ngawira uliofanywa katika
eneo la Minova mwezi Novemba mwaka jana.
Ulilishutumu jeshi la Congo kufanya
uhalifu huo.
Inaarifiwa maafisa 12 wa jeshi la
Congo walisimamishwa kazi kwa muda, lakini Umoja wa Mataifa unasema hakuna
aliyefikishwa mahakamani.
Chanzo: Dwswahili
No comments:
Post a Comment