TIDO MHANDO; Mwananchi haitarudi nyuma katika utendaji wake, Litaendelea kusimamia haki sheria na ukweli daima.
Tido Mhando
Mkurugenzi
mtendaji wa kampuni ya kuchapisha magazeti ya mwananchi Bw Tido Mhando amesema
licha ya kufunguiwa na serikali kwa kipindi cha wiki mbili haitarudi nyuma
katika utendaji wake na kuahidi kuendelea kusimamia haki sheria na ukweli
daima.
Mkurugenzi huyo ameyasema hayo alipokutana na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam akiwa kaambatana na mhariri mtendaji wa gazeti
la Mwananchi Bw Denis Msaki ambapo amesema kwa kipindi cha majuma mawili
wamepata hasara ya zaidi ya shilingi milioni 400.
Chanzo: ITV DAIMA
No comments:
Post a Comment