Kampuni ya Mwananchi Communications
Limited, wachapishaji na wauzaji wa magazeti ya MWANANCHI, MWANASPOTI, na THE
CITIZEN leo imetoa ufafanuzi katika mambo mawili, kuhusiana na tukio
lililotokea hivi karibu. Kwanza ni gazeti lake
mama la MWANANCHI ambalo halikuchapishwa wala kuuzwa kwa takribani majuma
mawili kwa agizo la serikali. Kuhusiana na hilo, wamechukua fursa na kuongelea kuhusu
KUREJEA KWA UCHAPISHWAJI WA GAZETI HILO na KUUSHUKURU UMMA kwa kuwa nao bega
KUREJEA KWA UCHAPISHAJI WA GAZETI
Kwa mujibu wa agizo la Serikali,
kutochapishwa kwa gazeti la Mwananchi kunakwisha leo, na kuanzia kesho tarehe
11.10.2013 gazeti litakuwa mitaani kama
kawaida. Kwa hiyo kuanzia kesho wasomaji wa gazeti hilo maarufu wataendelea kupata gazeti lenye
habari za uhakika zinazojikita kwenye umahiri, uhuru, na weledi wa uandishi na
uhariri.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni hiyo, Bw Tido Mhando, magazeti hayou yataendelea kusambazwa nchi nzima
na kufika mapema kabisa kote, kupitia kwa mawakala na wauzaji wake walioenea
kote Tanzania.
Kwa wapenzi wa gazeti la Mwananchi
waliopo jijini Dar es Salaam, kesho watauziwa
magazeti na waandishi wa gazeti hilo
ambao kuanzia asubuhi watakuwa mtaani wakisherehekea uhuru wao kwa kukutana na
wasomaji wao moja kwa moja.
PROMOSHENI YA CHOMOKA NA MWANANCHI
Kutochapishwa kwa gazeti la MWANANCHI
kwa majuma mawili kulisababisha ile promosheni ya CHOMOKA NA
MWANANCHI isimame kwa muda huo huo. Tido alichukua Fursa kuwajulisha
wasomaji wake kwamba promosheni hii sasa inarudi tena na inaendelea kuanzia
ilipokuwa imekomea.
Zawadi za shilingi milioni moja kila siku, na zawadi za magari mapya, zitaendelea kushindaniwa na kutolewa ili kutimiza ile ahadi yetu ya kutoa zawadi zenye thamani ya jumla ya shilingi 250,000,000/=.
PICHANI JUU:Mkurugenzi Mtendaji wa
Mwananchi Communications Limited(MCL)Tido Mhando akizungumza na waandishi wa
habari jijini kuhusu kuanza uchapishaji leo wa gazeti la Mwananchi lililokuwa
limefungiwa kwa wiki mbili.
Mkurugenzi wa Mwananchi, Tido Mhando
akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusiana na kuanza
kwa uchapishwaji wa gazeti hilo.
No comments:
Post a Comment