Ndege zisizokuwa na rubani maarufu Drones,zitapelekwa mashariki
mwa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo mwezi ujao. Ndege zisizo na rubani zijulikanazo kama
Drones.
Kamanda wa kijeshi wa tume ya kulinda amani ya umoja wa
mataifa nchini Kongo,Monusco amesema kwamba ndege hizo zitahusika na kuchunguza
mpaka wa Kongo na Rwanda.
Wakati huohuo shirika la kimarekani la Enough Project limetuhumu waasi wa M23
kuendelea na biashara haramu vya madini. Kwenye ripoti yake ilotolewa hii leo
shirika hilo limesema kila mwaka waasi hao na
washirika wao kutoka Uganda
na Burundi
wameuza dhahabu ya zaidi ya dola milioni mia tano.
Sikiliza taarifa kamili kutoka kwa mwandishi wetu Salehe
Mwanamilongo kwa bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Salehe MwanamilongoMhariri: Saumu Mwasimba
No comments:
Post a Comment