Picha za wanajeshi wa Kenya
waliokwenda katika jumba la Westgate katika juhudi za uokozi na kisha baadaye
kuonekena kwenye kamera za CCTV wakiondoka na mifuko ya plasitiki yenye bidhaa
za madukani, bila shaka zimewashangaza wengi.
Picha hizo mwanzo zimeonyesha
wanajeshi wakiingia ndani ya jengo hilo wakiwa wamebeba silaha kukabiliana na
wanamgambo walioshambulia jengo hilo wiki nne zilizopita na baadaye wakitoka
wakiwa wamebeba mifuko hiyo wakiwa na silaha zao kwa wakati mmoja.
Hata hivyo haijulikani walichokuwa
wamekibeba kwenye mifuko hiyo .
Pamoja na picha za wanajeshi wakiwa
wamebeba mifuko, pia kulikuwa na picha zengine zilizoonyesha mashine ya pesa
zikiwa zimeporwa ndani ya mikahawa huku picha za alama za risasi kwenye maeneo
ya kuhifadhia pesa, pia zikionekana.
Inaarifiwa ilikuwa jaribio ya
kufungua hifadhi hizo ambalo halikufanikiwa.
Madai haya ya wanajeshi kufanya
uporaji wa maduka katika jingo hilo, yalikanushwa vikali na jeshi la Kenya
kiasi cha kutaka hatua kuchukuliwa dhidi ya waliokuwa wanatoa madai hayo,
lakini haijulikani jibu lao litakuwa nini hasa kwa picha hizo za CCTV
zilizoonyesha wanajeshi hao wakifanya uporaji.
Wamiliki wa maduka waliorejea kwenye
maduka yao bbaada ya shambulizi , walidai kuwa maduka yao yaliporwa ingawa
jeshi lilikanusha madai hayo baadhi ya taarifa zikisema kuwa ilikuwa njama ya
wafanyabiashara kudai fidia kwa mali zao zilizoharibika.
Sio wanajeshi pekee waliotuhumiwa kwa
uporaji, kwani polisi mmoja naye alifikishwa mahakamani kwa kosa la uporaji
baada ya kupatikana na pochi la mtu liliokuwa na damu.
Wangambao wa Al Shabaab waliteka
nyara jengo la Westgate kwa siku nne na kusababisha vifo vya watu 60 pamoja na
kuwajeruhi zaidi ya watu miamoja.
Chanzo: BBCswahili
No comments:
Post a Comment