Hali ya sintofahamu inaonekana
kuunzunguka mkutano wa kimataida wenye lengo la kumaliza vita vya wenyewe kwa
wenyewe nchini Syria, kufuatia kauli zinazokinzana juu ya mkutano huo.
Jumuiya
ya Nchi za Kiarabu ilitangaza jana kuwa mazungumzo yatafanyika mwezi ujao
jijini Geneva, Lakini mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria Lakhdar Brahimi
amekanusha kuwepo kwa tarehe iliyopangwa kwa ajili ya mazungumzo hayo. Wakati
huo huo, nchini Syria kwenyewe watu 43 wameuawa katika shambulizi lililofanywa
na mlipuaji wa kujitoa mhanga.
Mkanganyiko
huo wa kidiplomasia ambao ni wa kushangaza, baina ya mkuu wa Jumuiya ya Nchi za
Kiarabu Nabil al-Arabi na Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Lakhdar Brahimi, katika
kikao cha pamoja cha waandishi wa habari mjini Cairo, unaendeleza mashaka juu
ya uwezekano wa kuandaliwa kongamano hilo la amani.
Mabaki
ya gari baada ya shambulizi la bomu la kujitoa mhanga mjini Hama, Syria Mabaki
ya gari baada ya shambulizi la bomu la kujitoa mhanga mjini Hama, Syria
Al-Arabi
alisimama na kutoa matamshi haya mbele ya waandishi wa habari "Nimejadili
suala la Syria na Lakhdar Brahimi na ikaamuliwa kuwa mkutano wa Geneva
utafanyika Novemba 23 na maandalizi yanaendelea kwa ajili ya kongamano hilo.
Yapo matayarisho mengi yakufanywa na vizuizi vingi ambavyo lazima viondolewe
kabla ya kuyafanyikisha mazungumzo hayo".
Kisha
ulipowadia muda wa Brahimi kuzungumza, akasema "Kuna makubaliano ya
kujaribu kuandaa kongamano la pili la Geneva mwezi Novemba kakini tarehe bado
haijatangazwa rasmi".
Brahimi
alionya kuwa mazungumzo hayo ya Geneva yataendelea tu ikiwa patakuwepo kile
alichokiita “upinzani halali unaoiwakilisha sehemu kubwa ya wananchi wa Syria”
ambao wanampinga Rais Assad. Alisema kuna makubaliano ya kuandaliwa mkutano wa
awamu ya pili jijini Gevena maarufu kama Geneva 2, lakini akaongeza kuwa tarehe
itatangazwa baadaye. Brahimi yuko katika mkondo wa kwanza wa ziara yake katika
Mashariki ya Kati inayolenga kutafuta uungaji mkono kwa mpango huo wa amani.
Amesema atazuru Qatar, Uturuki, Iran, Syria na kisha Geneva ili kufanya
mazungumzo na wawakilishi wa Urusi na Marekani, zikiwa ni nchi mbili
zilizoanzisha mpango huo.
Uamuzi
kama kweli mazungumzo hayo yaliyosubiriwa kwa hamu yatafanyika au la, huenda
ukatokana na mkutano wa upinzani nchini Syria mwezi ujao, ambao utajadili kama
utakaa kwenye meza moja na utawala wa Rais wa Bashar al-Assad. Nchini Syria
kwenyewe, gari lililokuwa na mabomu limelipuliwa na mlipuaji wa kujitoa mhanga
katika kituo kimoja cha kijeshi mjini Hama. Takribani watu 43 waliuawa ikiwa ni
pamoja na raia 32 huku wengine kadhaa wakijeruhiwa katika shambulizi hilo.
Shirika
la kutetea haki za binaadamu la Syria limesema wapiganaji wa kundi la Jabhat
al-Nusra ambalo lina mahusiano na mtandao wa al-Qaeda lilifanya shambulizi hilo
ambalo ni la pili kufanywa dhidi ya serikali katika siku mbili. Siku ya
Jumamosi, wapiganaji waasi wa al-Nusra walilipua bomu jingine wakati
wakikishambulia kituo kimoja cha serikali karibu na mji mkuu Damscus, na
kuwauwa wanajeshi 16.
Mwandishi:
Bruce Amani/AFP
Mhariri: Daniel Gakuba
No comments:
Post a Comment