Wanamgambo waliokuwa wamevaa nguo za
kijeshi, wamewaua watu 19 katika kuzuizi cha barabarani walichokuwa wameweka
kukagua magari katika jimbo la Borno.
Wanaume hao waliokuwa wamejihami ,
waliwasimamisha madereva na kuwaamrisha kuondoka kutoka katika magari yao kabla
ya kuwapiga risasi na kuwaua.
Walioshuhudia tukio hilo waliambia
BBC kuwa wanaume hao walikuwa wanachama wa Boko Haram, ingawa kundi hilo bado
halijatamka chochote kuhusu mauaji hayo.
Jimbo hilo la Kaskazini mwa Nigeria
liko chini ya sharia ya hali ya hatari, huku Boko Haram wakiwa vitani na
serikali kutaka utawala wa kiisilamu.
Kundi hilo huwalenga raia na
wanajeshi kwa mashambulizi ikiwemo shule na makabiliano ya mara kwa mara na
jeshi la taifa.
Shambulizi la hivi karibuni,
lilifanyika Jumapili, asubuhi karibu na mji wa Logumani, ambao hauko mbali sana
na mpaka na Cameroon.
Walionusurika shambulizi hilo
walisema kuwa washambuliaji walivaa nguo za jeshi na walikuwa wanaendesha
pikipiki kabla ya kuwashambulia waathiriwa.
"Takriban wanaume 9 walituamuru
kuondoka kwenye magari yeu na kulala chini,’’ alisema mwanamume
"Waliwaua watu 5 kwa kuwapiga
risasi na kasha kuwanyonga wengine 14 kabla ya mtu mmoja kuwapigia simu na
kuwambia kuwa wanjeshi wanakuja.’’
Alisema washambuliaji baadaye
walitoroka na kujificha msituni kwa pikipiki zao.
Manusura mwingine alisema kuwa
alisikia mtu aliyekuwa karibu naye akiuawa kwa kisu. Alisema ana uhakika kuwa
washambuliaji walikuwa Boko Haram kwa sababu ya kuwa na ndevu.
Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo alisema
kuwa ni jambo la kawida kwa polisi kuweka vizuizi barabarani hasa katika maeneo
yenye misukosuko na huenda washambuliaji waliiga mbinu hioyo ya jeshi ili
kuwanasa waathiriwa. I,
Boko Haram limezua mgogoro mkubwa wa
kisiasa Nigeria tangu mwaka 2009, nia yao kuu ikiwa kuunda utawala wa
kiisilamu, hasa katika maeneo ya kaskazini mwa nchi
Kundi hilo limelaumiwa kwa
mashambulizi kadhaa ambao yamesababisha takribna vifo 2,000 tangu mwka 2011.
Chanzo: BBCSwahili
No comments:
Post a Comment