Watu watatu akiwemo msichana mdogo
mwenye umri wa miaka 8 aliuawa wakati watu waliokuwa wamejihami wakiwa kwenye
pikipiki kushambulia sherehe za ndoa nje ya kanisa la Kikopti mjini Cairo.
Takriban wengine 9 walijeruhiwa
kwenye shambulizi hilo mjini Giza.
Hata hivyo hakuna taarifa zozote
kuhusu nani aliyehusika na shambulizi hilo.
Jamii ya wakristo wa kikopti wamekuwa
wakishambuliwa na baadhi ya waisilamu wanaotuhumu kanisa kwa kuunga mkono jeshi
katika kumpindua aliyekuwa Rais Mohammed Morsi mwezi Julai.
Washambuliaji hao ambao
hawakutambuliwa, waliwafyatulia risasi kiholela watu waliokuwa wanaondoka
kanisani.
Mwanamume mmoja na mtoto huyo
waliuawa nje ya kanisa hilo wakati mwanamke mmoja akifariki akipelekwa
hospitalini.
"Tulisikia mlio mkubwa sana
mfano wa kitu kilichokuwa kinaanguka,’’ alisema shahidi mmoja.
"Nilimkuta mwanamke mmoja akiwa
ameketi kwenye kiti chake, akiwa amejeruhiwa kwa risasi. Watu wengi walikuwa
wameanguka kando yake akiwemo mtoto mdogo.’’
Kasisi wa kanisa hilo Thomas Daoud
Ibrahim alisema kuwa alikuwa ndani ya kanisa hilo, wakati, milio ya risasi
ilikuwa inasikika.’’
"Kilichofanyika ni kitu kibaya
sana na sio waksristio wakopti waliolengwa pekee yao , tunaharibu nchi yetu,’’
alisema kasisi huyo.
Kasisi mwingine aliambia vyombo vya
habari kuwa kanisa hilo liliachwa bila polisi wala mlinzi tangu mwishoni mwa
mwezi Juni.
Kanisa hilo ni moja ya makaisa ya
zamani ya kikristo iliyoanzishwa mjini Alexandria mapema miaka ya 50 AD.
Idadi ya wakristo nchini Misri ni
asilimia 10 ikiwa waumini milioni 80, na wamekuwa wakiishi kwa amani na
waisilamu wa kisunni kwa miaka mingi.
Hata hivyo, kuondolewa mamlakani kwa
Morsi kijeshi, kumefuatiwa na mashambulizi mabaya dhidi ya makanisa na
rasilimali za waumini hao kwa miaka mingi.
Wakati mkuu wa majeshi Generali,
Abdul Fattah al-Sisi, alitangaza kwenye televisheni kuwa rais Morsi aliondolewa
mamlakani baada ya maandamano makubwa yakimtaka ajiuzulu aliandamana na papa
Tewadros.
Tewadros alisema kuwa mkakati
uliofikiwa na Al-asisi ulitokana na mawazo ya viongozi waheshimiwa ingawa
hakuwataja.
Chanzo: BBCSwahil
No comments:
Post a Comment