Madereva na Mafundi wa Treni za
TAZARA wakiwa katika moja ya vichwa sita vipya vya Treni ambavyo vimeletwa Tanzania na
wapo katika mafunzo ya jinsi ya kuvitumia. (HM)
SHIRIKA la reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) limepata vichwa sita
vya Treni vipya kutoka nchini China
vyenye uwezo wa kubeba tani 1800 kila kimoja.
Kufuatia kutolewa kwa vichwa hivyo
vya Treni vipya, madereva 160 na mafundi 80 wa karakana ya Treni Iyunga mkoani
Mbeya wanapatiwa mafunzo yakakayo wawezesha kufanya kazi kwa umakini katika
vichwa hivyo.
Akitoa maelezo ya ujio wa vyicho
hivyo Mhandisi Mwandamizi katika karakana na Iyunga Eng. Davie Tembo alisema
kuwa vichwa hivyo vya treni vyenye uwezzo wa kubeba Tani 1800 vimeletwa Juzi
katika karakana hiyo.
Alisema kuwa vimetoka nchini china na
ni toleo jipya ambalo linahitaji madereva na mafundi kujifunza kabla ya kuanza
kutumia kwani linatumia mfumo mpya.
Tembo alisema kuwa kampuni ya CSR
Qishuyan ya nchini China
ndio iliyo tengeneza vichwa hivyo na inatoa mafunzo kwa madereva na mafundi
jinsi ya kuvimudu vichwa hivyo.
Alisema kuwa wamevijaribu vichwa
hivyo na kuviona vinafaa kwa matumizi na havina shida yoyote.
Awali akifungua mafunzo kwa madereva
hao Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA, Said Sauko alisema kuwa mafunzo hayo
yatalenga kwa Wafanyakazi wa TAZARA watakao kuwa katika makundi saba ambapo
kila kundi litakuwa na watu wasio pungua 40.
Alisema kuwa mafunzo hayo yatatolewa
kwa muda wa mwezi mmoja na yamelenga kwa wafanyakazi kutoka Tanzania na Zambia. Chanzo: Furahia Eliab, Mbeya
No comments:
Post a Comment