Aliyekuwa Rais wa Misri Mohammed
Morsi aliyeng'olewa mamlakani atafunguliwa mashtaka mwezi Novemba tarehe nne.
Bw Morsi atashatakiwa kwa kosa la
uchochezi na mauaji pamoja na wanachama kumi na wanne wa kundi Muslim
Brotherhood.
Mashtaka hayo yanahusiana na mauaji
ya waandamanaji saba wakati wa vurugu kati ya wafuasi wa upinzani na wafuasi wa
Muslim Brotherhood nje ya ikulu ya rais mjini Cairo mwaka uliopita.
Kupinduliwa kwa bwana Morsi
kumesababisha maandamano ya kupinga na kumuunga mkono kutoka kwa wafuasi na
wapinzani na wafuasi wake na baadhi wameuawa na vikosi vya kijeshi.
Morsi atashtakiwa na viongozi wengine
kumi na wanne wa vuguvugu la Brotherhood.
Amekuwa akizuiliwa katika eneo
lisilojulikana tangu alipoondolewa mamlakani tarehe 3 mwezi Julai.
Mamia ya watu wanataka arejeshwe
mamlakani na wengi wao wakiwa wafuasi wa vuguvugu la Brotherhood. Wengi wa
wafuasi hao wameuawa kwenye makabiliano na vikosi vya usalama tangu Morsi
alipong'olewa madarakani.
Zaidi ya watu hamsini walifariki
kutokana na ghasia hizo siku ya Jumapili.
Mahakama ya rufaa mjini Cairo iliamua kuwa Morsi
na wenzake 14 akiwemo Mohammed al-Beltagi na Essam al-Erian, wanaweza
kufunguliwa mashtaka katika mahakama ya uhalifu.
Wendesha mashtaka walitangaza kuwa
mwezi jana walifunguliwa mashtaka ya uchochezi kuhusiana na ghasia nje ya ikulu
ya Rais mjini Cairo.
No comments:
Post a Comment