Na Darlin Said
Waziri
Mkuu , Bw. Mizengo Pinda , amesitisha utekelezwaji wa agizo la Waziri wa
Ujenzi, Dkt. John Magufuli la kuondoa msamaha wa tozo kwa uzito wa magari
uliozidi ndani ya asilimia tano ya uzito unaokubalika kisheria.
Bw. Pinda alitoa uamuzi huo Dar es Salaam jana siku moja
baada ya Chama cha Wamiliki wa Malori nchini (TATOA), kutangaza uamuzi wa
kupaki magari yao wakipinga agizo hilo.
TATOA pamoja na Chama wa Wamiliki wa Mabasi yaendayo Mikoani
(TABOA), walipinga agizo la Dkt. Magufuli kutaka magari yanayobeba uzito wa
tani tatu na nusu na kuendelea, kupimwa mizani bila msamaha wa tozo uliozidi ndani
ya asilimia tano ya uzito uliokubaliwa kisheria.
Alisema kutokana na sakata hilo, amelazimika kuunda kamati ambayo
itakutana na wadau TATOA na TABOA ili kupata ufumbuzi wa mgogoro uliojitokeza.
"Kwa kuwa bado kuna mgogoro kati ya Wizara ya Ujenzi, Wasafirishaji
wa malori na mabasi kuhusu utekelezwaji wa kanuni 7(3), ambao wanasema
haitekelezeki kirahisi, naiagiza Wizara ikutane na wadau. "Wakae na
kujadili namna bora ya kutekeleza kanuni hii, Wizara ya Ujenzi na Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, waunde timu ya wataalamu ambao watakutana na
wawakilishi wachache wa TATOA na TABOA ili wapitie kanuni hizi kwa lengo la
kupata mwafaka," alisema Bw. Pinda.
Aliongeza kuwa, mwezi mmoja unatosha kwa Wizara na wadau
hao, kukamilisha kazi hiyo na utaratibu uliokuwepo awali kabla ya tangazo la
Serikali uendelee kutumika.
Aliitaka Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kupanga
utaratibu mzuri wa kupima magari hayo katika mizani ili kuondoa msongamano
katika kituo kimoja.
"Wakati umefika kwa Wizara husika kukagua mizani na
kuangalia ubora wake kwani hicho ndio chanzo kikuu cha mgogoro uliopo... baadhi
ya watumishi katika mizani si waaminifu, wanapokea rushwa hivyo Wizara iangalie
namna ya kutatua tatizo hili," alisema.
Akizungumzia
barua iliyoandikwa mwaka 2006 na Waziri wa Miundombinu (wakati huo), Bw.
Basil Mramba. Barua hiyo ilitoa nafuu ya punguzo la asilimia tano ya uzito wa
'Axel' za magari utakaosomwa kwenye mizani ili kufidia kasoro za mizani
kutopima kwa usahihi uzito wa magari.
Alisema
msamaha huo ulikuwa kinyume na Sheria ya Usalama Barabarani, sura ya 168, toleo
la 2002 na kanuni zake za mwaka 2001 za Usalama Barabarani juu ya ukomo wa
uzito wa magari.
"Ingawa
Bw. Mramba alifanya hivyo kwa nia njema, wasafirishaji wakatumia fursa hiyo
vibaya kwa kuongeza mizigo kwenye magari yao
kwa sababu kuna msamaha wa asilimia tano," alisema.
Bw.
Pinda alisema, kutokana na hali hiyo Dkt. Magufuli aliamua kufuta muongozo wa
barua hiyo na kujielekeza katika sheria na kanuni za Usalama Barabarani za
mwaka 2001.
Sheria
hiyo inasema uzito uliozidi lakini upo ndani ya asilimia tano ya uzito
unakubalika kisheria, magari hayo yanapaswa kupunguza mzigo, kupanga mzigo na
ikishindikana watatakiwa kulipia uzito mara nne ya tozo ya kawaida.
Awali
Bw. Pinda alisema, Serikali haitaruhusu malori na mabasi kuzidisha mizigo kama nafuu wanayoitafuta kwani barabara zilizopo zina
uwezo wa kudumu miaka 20 kwa magari yaliyobeba uzito unaokubalika kisheria.
mzia mgogoro huo, Bw. Pinda alisema chanzo chake ni baada ya Dkt. Magufuli
kufuta
Chanzo: Majira
No comments:
Post a Comment