Shirikisho la Soka la Dunia (Fifa)
limetangaza viwango vipya vya ubora wa soka kwa Oktoba, huku Tanzania
ikiporomoka kwa nafasi mbili kutoka ile ya 128 hadi 130.
Licha ya kuporomoka, pia Tanzania
imejikuta ikikamata mkia kwa ubora wa soka miongoni mwa nchi tano za Jumuiya ya
Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, Uganda
imeteremka kwa nafasi nne kutoka 81 hadi 85, hata hivyo imeendelea kushikilia
rekodi ya nchi inayoongoza kwa ubora kati ya nchi tano za Afrika Mashariki.
Nchi nyingine zinazounda jumuiya hiyo
na viwango vyao vya ubora ni Ethiopia iliyoshuka kwa nafasi mbili kutoka 93
hadi 95, Kenya nafasi ya 118, wakati Burundi imepanda kwa nafasi mbili kutoka
120 hadi 122 na Rwanda ambayo pia imechupa kwa nafasi mbili kutoka 129 hadi
131.
Ivory Coast imeendelea kukaa kileleni
ikishikilia nafasi ya kwanza kwa ubora wa soka Afrika, huku ikipaa kwa nafasi
mbili kutoka 19 hadi 17, wakati mabingwa wa Afrika, Nigeria wakiwa
wamejitutumua na kupanda kwa nafasi tatu kutoka 36 hadi 33.
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment