Uamuzi
huu umetolewa huku AU ikifanya juhudi za kidiplomasia kutaka kesi hiyo
kuahirishwa kwa mwaka mmoja
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC
imeahirisha kesi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika mahakama hiyo hadi
tarehe 5 mwezi Februari mwaka 2014.
Uamuzi huo umefikiwa hii leo ikiwa
siku moja kabla ya upande wa mashitaka kuashiria kuwa hawatapinga ikiwa kesi
hiyo kuahirishwa kwa mwaka mmoja hadi Novemba mwaka 2014
Pia unakuja huku juhudi za
kidipmolasia za viongozi wa Afrika kushinikiza baraza la usalama la Umoja wa
Mataifa zikishika kasi kulitaka baraza hilo kukubali kesi dhidi ya Rais
Kenyatta na naibu wake William Ruto kuakhirishwa.
Rais Kenyatta alikuwa ameiomba
mahakama hiyo kuakhirisha kesi dhidi yake hadi Februari mwaka ujao huku upande
wa mashitaka ukitaka ukahirishaji kutozidi Februari tarehe tatu mwaka 2014.
“Majaji wamekubaliana na upande wa
mashitaka kuahirisha kesi dhidi ya Rais Kenyatta hadi Februari mwaka 2014 ili
kuupatia upande wa mashitaka muda wa kutosha kufanya uchunguzi zaidi kutokana
na tuhuma dhidi ya upande wa mashitaka kutoa taarifa zisizo za kweli, '' majaji
walisema katika uamuzi wao.
Upande wa utetezi nao ulitaka tarehe
ya kesi hiyo kuahirishwa ili majaji waweze kushughulikia baadhi ya malalamiko
yao, kuhusu Kiongozi wa mashitaka kuhujumu mfumo wa kesi dhidi ya Kenyatta.
Malalamiko hayo waliyawasilisha Oktoba tarehe kumi na kuwasilisha ombi la
kutaka kesi dhidi ya Rais Kenyatta kufutiliwa mbali.
Chanzo: BBCSwahili
No comments:
Post a Comment