Kiongozi wa wapiganaji wa M23 mashariki
mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo ametangaza kuwa watasitisha mapigano katika
vita vyao na jeshi la serikali.
Bertrand Bisimwa alisema kwenye
taarifa kwamba anawasihi wapiganaji wote haraka waache uhasama na wanajeshi,
ili kuwezesha mazungumzo ya amani kuendelea.
Wanajeshi wa serikali, wakisaidiwa na
kikosi cha kuweka amani cha Umoja wa Mataifa, hivi karibuni wamewasukuma nyuma
wapiganaji na kuwatoa katika ngome zao nchini.
Mazungumzo ya amani yanafanywa mjini
Kampala, Uganda.
Chanzo:
BBCSwahili
No comments:
Post a Comment