Shughuli
ya kutia saini mkataba wa amani kati ya waasi wa M23 na serikali na Jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo,iliyokukuwa imepangwa kufanyika Jumatatu , iligonga
mwamba.
Hii
ni kutokana na serikali ya Congo kusema kuwa mkataba huo uangaliwe upya na
hivyo kulazimisha shughuli hiyo kuahirishwa.
Mpatanishi
wa pande hizo mbili Ofuono Opondo wa Uganda, alisema kuwa pande hizo hazikuwa
tayari kuonana ana kwa ana baada ya DRC kusema kuwa M23 watie saini mkataba
katika chumba tofauti na kisha wapewe wao kuusaini.
Hata
hivyo mpatanishi alisema haiwezekeni kwa hilo kufanyika kwa sababu pande
zinazozozana lazima zikae katika chumba kimoja kwa ajili ya kufanikisha juhudi
za upatanishi.
Kundi
la waasi la M23 lilisitisha uasi wao baada ya kupata kipigo kutoka kwa
wanajeshi wa DRC wakisaidiwa na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa waliowafurusha
kutoka maficho yao ya milimani katika mpaka wa Rwanda na Uganda.
Mkataba
huo ulistahili kutiwa saini mjini Kampala Uganda, ingawa shughuli yenyewe
ilicheleweshwa bila ya kujua itafanyika lini.
Mwandishi
wa BBC mjini Kampala, Ali Mutasa anasema kuwa mpatanishi mkuu Ofwono Opondo
alisema mkataba hautatiwa saini na kwamba haijulikani ni lini makubaliano hayo
yatasainiwa. Alisema Upande wa M23 uko tayari kwa shughuli hiyo na kuwa
kizungumkuti kimetokana upande wa DRC.
Serikali
ya DRC kupitia kwa msemaji wake,Lambert Mende ilisema kuwa Kinshasa iko tayari
kutia saini makubaliano hayo, lakini sio mkataba unaosema ni makubaliano ya
amani kwa sababu ni kama kundi hilo bado lipo.
Duru
zinasema kuwa Rais Yoweri Museveni pamoja na wanadiplomasia wa nchi za
Magharibi, walisburi mkataba kutiwa saini lakini wajumbe wa DRC hawakuingia
katika chumba cha hafla hiyo ya kutia saini.
No comments:
Post a Comment